WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA TAWI LA PBZ MOROGORO,ASISITIZA FULSA KWA VIJANA ELIMU YA JUU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 9 July 2024

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA TAWI LA PBZ MOROGORO,ASISITIZA FULSA KWA VIJANA ELIMU YA JUU

 






Na Lilian Kasenene,Morogoro 

maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameitaka Bank ya watu wa Zanzibar (PBZ)kutoa fursa kwa vijana wa vyuo vya elimu ya juu nchini, hususani wale wasiokuwa na uwezo, kupata mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya masoko yao.


Waziri mkuu amesema hayo Leo July 9 mjini Morogoro  wakati wa uzinduzi wa tawi la PBZ.


Pia amesema  uwepo wa tawi la benki ya watu wa Zanzibar mjini Morogoro kutaongeza chachu kwa wananchi kupata mikopo itakayo wawezesha kujiajiri katika sekta za kilimo na biashara.


Aidha alisema benk hiyo imepata mafanikio ikiwemo kutoa mikopo ya shilingi bilioni sita kwa wakulima 3,011 hadi kufikia Juni 30 kwenye matawi yake yote.


Alisema  benki hiyo inamchango mkubwa  katika  kuunga mkono juhudi za serikali zote mbili  kwa kuwawezesha mikopo wakulima ambapo alitolea mfano  wa mwani pamoja na kukoleza uchumi wa bluu.


"Kwa sasa wajasiliamali wabuni biashara mbalimbali, mikopo ipo" alisema.

Kwa upande wa Bank hiyo aliiwataka kutoa elimu juu ya mikopo wanayotoa na urejeshwaji wa mikopo ,,  usimamizi  wa mikopo, ufafanuzi juu ya riba ili iwasaidie wananchi kupata maslai kupitia mikopo hiyo.


Kwa  upande wa wananchi aliwataka  kuhakikisha wanafuata  wanasoma na kuelewa masharti na kanuni za mikopo  na kuzingatia kurejesha  kwa mujibu wa sheria.


Naye mkurugenzi mtendaji wa Bank ya watu wa Zanzibar PBZ Arafat Haji alisema kuanzishwa kwa tawi hilo mkoani Morogoro  kutaimarisha  usalama wa fedha kwa wafanyabiashara wanaotoka Zanzibar kuja kununua bidhaa huku na vile vile wanaokwenda Zanzibar kununua bidhaa.


"Kwa sasa wafanyabiashara hawatakuwa na sababu ya kubeba fedha nyingi na  badala yake watatumia bank hiyo" alisema.


Alisema hadi sasa wameshafungua matawi katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam , Mtwara na  mbeya ambapo wana mpango wa kufungua matawi mengine katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Tanga ambapo hadi sasa wana mawakala 1326 nchi nzima.


Alisema ufunguzi wa tawi hilo ni shamrashara za kufikisha miaka 58 ya bank hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1966.


Kwa upande wake Dionisia  Mjema Kamishna msaidizi wa idara ya  maendeleo ya sekta ya fedha wizara ya  fedha  alisema bank hiyo  ina maendeleo  na kwamba ni ya saba kati ya mabenk 44 yaliyopo nchini.


Alisema uwepo wa bank hiyo itasadia kupanua wigo wa biashara  kati ya Zanzibar na Morogoro na hivyo kuleta tija kwa taifa.


Naye waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili Zanzibar Hamza Hamis Jumaa alisema wapo wakulima wengi  wa  Zanzibar  wanalima mpunga mkoani Morogoro  na kupeleka Zanzibar na kule Zanzibar kuna eneo maalum wapo wananchi wa Morogoro ambao ni Waruguru wanafanya shughuli zao hivyo Zanzibar na Tanzania Bara ni washirika katika masuala mbalimbali.





No comments: