Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Apongeza ushirikiano wa wanahabari na Polisi Manyara - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 8 August 2024

Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Apongeza ushirikiano wa wanahabari na Polisi Manyara

 

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Sharlotte Ozaki akizungumza na waandishi wa mkoa wa Manyara

Mkurugenzi wa Muungano wa vlabu vya waandishi wa habari Tanzania ( UTPC) Kenneth Simbaya akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara 



Na Mwandishi Wetu, maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Balozi wa Sweden nchini Tanzania Sharlotte Ozaki Mercias amelipongeza Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa wanahabari pamoja na kazi nzuri zinazofaywa na waandishi wa Habari ndani ya mkoa huo.


Ametoa pongezi hizo alipotembelea klabu ya waandishi wa habari Mkoa Manyara mjini Babati mapema Jana.


Aidha Serikali imeshauriwa kujenga nyumba salama katika maeneo mbali mbali nchini kwaajili ya kuwahifadhi watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa na kulawitiwa ili kuzuia mazingira ya kupoteza ushahidi wa kesi kufikishwa mahakamani. 


Ushauri huo umetolewa na Afisa wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Manyara Maige Kulwa mbele ya klabu ya waandishishi wa habari walipotembelewa na Balozi wa uswizi  nchini Tanzania Sharlotte Ozaki Mercias ambae anafanya ziara ya kutembelea klabu za waandishi kuona namna gani klabu hizo zinafanya kazi.


 Amesema baada ya vitendo vya kikatili kufanyika wanafamilia wanakua karibu na waliowafanyia vitendo hivyo na kuficha ukweli huku wakitaka kesi hizo zizungumzwe kifamilia na bila kufikishwa mahakamani.


"Kwasababu makosa mengi sana yanapatanishwa kijamii na Kesi  zinashindwa kufika mahakamani, tulimpata muathirika wa vitendo vya ukatili na kuhifadhiwa nyumba salama itasaidia kesi kwenda kwa haraka na ushahidi kamili".


 Mkurugenzi wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania ( UTPC) Kenneth Simbaya amesema, katika suala la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Jeshi la polisi linapaswa kushirikiana kwa ukaribu na  waandishi wa habari kwa kusaidia kuibua  na kutoa taarifa zilizojificha ili ziweze kushughulikiwa. 



" Jeshi la polisi lipo kwaajili ya kulinda usalama wa Raia, na Waandishi ni miongoni mwa raia,tunasisitiza ushirikiano kama huu uigwe na makamanda wengine nchini mwandishi hapaswi kufanya kazi kwa hofu".



"UTPC itaendelea kuwajengea uwezo klabu za waandishi wa habari ili ziweze kuandika habari zenye maslahi kwa uma lakini pia kusukuma uwajibikaji ".


Amesema,katika suala la uchaguzi, waandishi wa habari wanawajibu wa kuwaelimisha wananchi namna ya kujiandikisha, na kuwaelezea wananchi kuchagua viongozi bora ambao watakua na maslahi kwa Taifa.

 

No comments: