TBS YAWATAKA WAJASILIAMALI WADOGO KUANZIA SIDO ILI KUPATA HUDUMA BURE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 7 August 2024

TBS YAWATAKA WAJASILIAMALI WADOGO KUANZIA SIDO ILI KUPATA HUDUMA BURE




Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com 


SHIRIKA la viwango Tanzania(TBS) limewataka wajasiliamali wadogo kabla ya kufika kwao kupata huduma wahakikishe wanaanzia  shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO kjiandikisha ili kuweza kupata huduma ya kuthibitishiwa ubora wa bidhaa zao bure kwa muda wa miaka mitatu.


Kaimu meneja wa TBS  Kanda ya mashariki Francis Mapunda alisema hayo katika maonyesho ya nanenane kanda ya mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro. 


Alisema kwa sasa wengi wa wajasiliamali wameanza kuelimika na tunapp0elekezwa kuwa huduma hiyo  inatolewa "bure wanaridhika na wameanza kwenda kujiandikisha


'Tuna makundi ya watu wote kuna ambao tayari ni waelewa walishajaribu huduma zetu na kuna ambao ni wajasiliamali wadogo wanakuja mara ya kwanza na tukiwaelekeza wapitie SIDO wakishaandikishwa  sisi tunatoa huduma uthishaji wa ubora bure wanaenda kujiandikisha," alisema Mapunda


Aidha meneja huyo alieleza athari za bidhaa duni ambazi hazijafikia viwango kuwa ni kuathiri afya ya watumiaji na kuharibu soko ya bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya nje.


Mapunda alisema bidhaa duni pia inaharibu ushindani wa kibiashara kwenye soko kwani bei yake inakuwa ni ya chini ikilinganishwa na bidhaa zenye ubora.


TBS iliwashauri wazalishaji wadogo wafike kwenye shirika hilo ili kupata huduma ya ubora na pia kupata ushauri wa kitaalam pale bidhaa zinaonekana kuwa na changamoto ya viwango  vya  ubora...


Alisema TBS inapima bidhaa zote za kilimo, mifugo wavuvi kwenye maabara ili kuhakikisha zinakidhi viwango vinavyotakiwa.


Alisema pia wanatoa mafunzo kwa wajasiliamali, wazalishaji,na wasindikaji ili kuhakikisha wanzalishaji bidhaa salama na bora kwa afya ya mlaji na zinakidhi matakwa ya viwango. 


Mmoja wa wajasiliamali walionufaika na huduma hiyo Joyce Jackson ambaye ni msindikaji wa viungo vya chakula alisema baada ya kupata cheti cha ubora wa bidhaa zake imemsaidia kuweza kupeleka bidhaa zake hadi nje ya nchi.


"Kuna wakati nilipata nafasi ya kushiriki maonyesho ya Afrika Mashariki lakini nilishindwa kuuza bidhaa zangu kwani wateja waliokuwa wanakuja bandani kwetu walikuwa wanahitaji nembo ya  uthibitisho wa viwango vya ubora na wasipoina kwenye kifungashio wanaondoka,"alisema Joyce.


Mwisho.

No comments: