Bandari ya Tanga yapokea meli kubwa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 1 August 2024

Bandari ya Tanga yapokea meli kubwa





Na: Burhani Yakub, Tanga.

maipacarusha20@gmail.com 

Bandari ya Tanga imeingia katika historia mpya baada ya kupokea meli kubwa ya yenye shehena ya mizigo yakiwamo magari 500 ikiwa na tani 14,000 kutoka nchini China.


Meli hiyo ya MV ANNEGRIT ikiwa chini ya kampuni ya uwakala ya Seafront Shipping Service (SSS) iliwasili katika Bandari ya Tanga na kupokewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga,Balozi Batilda Buriani.


Meneja Mkuu wa Kampuni ya uwakala wa Meli ijulikanayo SSS,Neelakandan Jambulingam amesema meli hiyo mbali ya kuwa na sehena ya bidhaa tofauti pia ina magari zaidi ya 500 ambayo itapelekwa nchi za Zambia, Zimbabwe,Jamhuri ya Watu wa Congo DRC,Malawi,Rwanda na nchi nyingine za Maziwa Makuu.


Mwezi ujao Seafront Shipping Service tutaleta shehena kuputia Bandari hii ya Tanga ambapo kati ya meli keep kubwa kuanzia tatu hadi nne zitawasili na kupelekwa nchi za Maziwa Makuu na maeneo mengine"amesema Neelakandan.


Naibu Waziri wa Uchukuzi,. David Kihenzile amesema Serikali imetambua umuhimu wa Bandari ya Tanga kwa kuchimba kina na kuipanua ili kuwezesha kutia nanga meli kubwa Duniani.


"Kwa uwekezaji huu uliofanywa na Serikali wa kuchimba kina kutoka mita tatu hadi 13 na kuipanua hadi mita 73 kwa sh 429.bilioni ni wazi kuwa bandari hii itakuwa na uwezo mkubwa kupokea meli za ukubwa wowote Duniani"amesema Kihenzile.


Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini na nchi za Maziwa Makuu kuitumia bandari ya Tanga kwa kuwa inatoa huduma kwa haraka.


"Nitoe wito kwa wafanyabiashara wa ndani na nchi za jirani itumieni bandari ya Tanga kwani ina uwezo wa kutoa huduma kwa haraka "amesema Buriani.


MWISHO

No comments: