JESHI LA ZIMAMOTO MANYARA LAOKOA MATUKIO 44 YA MOTO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 2 August 2024

JESHI LA ZIMAMOTO MANYARA LAOKOA MATUKIO 44 YA MOTO



Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara Gilbert Mvungi



Na Epifania Magingo,Babati


maipacarusha20@gmail.com

Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara limewata wananchi wa Mkoa huo na maeneo mbalimbali nchini kuzingatia elimu inayotolewa na jeshi hilo kwa njia mbalimbali ya namna ya kujikinga na majanga ikiwemo ya moto.


Elimu inayotolea na Jeshi hilo ni ya nadharia na vitendo na kwamba kuna vifaa maalumu vinavosaidia kuzima moto katika hatua za awali kabla haujawa mkubwa.

Akizingumza na Mwandishi wa maipac Media ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara Gilbert Mvungi amesema jengo likiwa limeshika moto na watu wakiwemo ndani hawapaswi kutoka nje wakiwa wima kwakua wanaweza kupata madhara makubwa.

Amesema kunapotokea hitilafu ya moto ndani ya jengo watu waliomo wanapaswa kutoka nje kwa kutambaa na Kisha kutoa taarifa ya idadi ya waliomo ndani ya jengo ili shughuli ya uokoaji iweze kufanyika kwa haraka.

"Ukienda wima utavuta moshi mkali,utavuta hewa ya kabobimonoxide ambayo itakwenda kudhuru mfumo wa fahamu utaanguka,utapoteza maisha".

Akitoa takwimu za matukio ,Kamanda Gilbert amesema matukio yaliyoripotiwa ni 105 ambapo matukio ya moto ni 61 na matukio ya maokozi ni 44.


Amesema kila mwananchi anahaki ya kutoa taarifa ya matukio ya majanga kwa Jeshi hilo ili kupata msaada kwa namba 114 ambayo ni bure huku akisistiza kuwa mwananchi anapaswa kujieleza kikamilifu mahali alipo na tukio gani limetokea kwa wakati huo.


Kamanda Gilbert amesema Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Manyara limefanikiwa katika shughuli zake za kutoa huduma kwa wananchi kwa kutoa elimu na kuwajengea uwezo wananchi jinsi ya kujikinga na majanga mbalimbali ikiwemo ya moto na kwamba Serikali imeongeza jitihada ya kununua vitendea kazi ikiwemo kuongeza gari la zimamoto ambapo kwasasa yako mawili.


"Tunatoa elimu katika maeneo mbalimbali kupitia vyombo vya habari,sehemu za mikusanyiko,katika mashule,vituo vya mabasi, bodaboda, makanisani, msikitini".


Amesema, wamefanaya ukaguzi na kutoa ushauri katika majengo mablimbali pamoja na kupitisha michoro inayoletwa kutoka kwa wananchi na kutoa ushauri jinsi ya kuweka vifaa vya kijikinga na majanga ya moto.


"Tunashauri kitaalamu kulingana na jengo husika namna ya kuweka vifaa vya kudhibiti moto,kwamba hapa utaweka kifaa hiki Cha moto na hapa hiki".


Amesema kuna mfumo wa kugundua moto, mfumo wa kuashiria hatari ya moto ndani ya jengo na kuna mfumo wa watu kupitia kutoka nje ndani ya jengo pindi hatari ya moto inapotokea.



No comments: