MCHUNGAJI WA MIFUGO AFUNGWA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MIWILI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 30 August 2024

MCHUNGAJI WA MIFUGO AFUNGWA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MIWILI

 



Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Mahakama ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara imemuhukumu Mchungaji wa mifugo Carol Christopher (18)mkazi wa kijiji Cha Moringe Wilayani Mbulu kutumikia kifungo Cha maisha yake yote Gerezani baada ya kumkuta na hatia ya kumwingilia mtoto mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane na kumlawaiti.


Hukumu hiyo imetolewa huku Mshtakiwa akiwa ametoroka na mama yake Anna Burra aliyekuwa amemdhamini akihukumiwa kifungo Cha miezi sita Gerezani baada ya kushindwa kulipa fungu la ahadi ya shilingi milioni 3 ya dhamana aliyokuwa amemuwekea mtoto wake Carol, huku pia akiidanganya Mahakama kuwa Mshtakiwa amelazwa katika hospitali ya Seliani Mkoani Arusha na kushindwa kutoa vielelezo  Mahakamani.


Upande wa Jamhuri ulioongozwa na Mkaguzi wa Polisi Maraba Masheku uliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu Kali itakayokuwa funzo kwa jamii akitilia msisitizo kuwa Serikali ikitumia nguvu kubwa kukemea na kutoa Elimu kwa kuzingatia kifungu Cha Sheria 154 (2) Sura ya 16, lakini pia mlalamikaji akiwa mtu mzima na mlalamikaji akiwa Chini ya umri wa miaka 10.


Akitoa hukumu Huku Mahakama hiyo ikiwa tayari imetoa hati ya kumtafuta mshatikiwa Carol ili afike Mahakamani kusomewa shtaka lake, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mheshimiwa Johari Kijuwile amesema hukumu hiyo imezingatia Upande wa utetezi wa mashahidi  wanne kushindwa kuithibitisha Mahakama hiyo, lakini pia Upande wa Mashtaka uliowasilishwa na mashahidi sita ikiithibitishia ukatili aliotendewa mtoto huyo.


Hakimu Kijuwile amesema japokuwa shahidi namba Tano ambae ni mtoto mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane na hakuweza kuongea lakini Mahakama imetumia busara ya kuzingatia maoni na kwakuzingatia hilo imelazimika kutoa hukumu ya kifungo Cha maisha Gerezani.


 Hata hivyo,Kijowile amesisitiza kutoa hukumu hiyo katika mazingira ya kutokuwepo Carol kwakua alikua Akihudhuria kwenye shauri hilo mpaka siku ya utetezi wake lakini hakuweza kuhudhuria mara mbili kwenda kusikiliza hukumu yake hata pale Mdhamini wake alipotakiwa kutoa vielelezo alishindwa kufanya hivyo na kuonekana kuwa anaidanganya Mahakama hiyo kwakua hakuonekana Mahakama imetoa hati ya kumtafuta na kumkamata ili afikishwe kusomewa hukumu hiyo na adhabu itaanza pale tu atakapokamatwa.

No comments: