MKUFYA ATETEA NAFASI YAKE MAKAMU MWENYEKITI CHALINZE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 30 August 2024

MKUFYA ATETEA NAFASI YAKE MAKAMU MWENYEKITI CHALINZE







Na: Julieth Mkireri, Maipac CHALINZE




maipacarusha20@gmail.com


MADIWANI wa Halmashauri ya Chalinze wamemchagua Ramadhani Mkufya kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao baada ya kumaliza awamu yake ya kwanza.


Mkufya amechagukiwa kwa kura 17 za ndiyo kati ya Madiwani 17 walioshiriki kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.


Katika Baraza hilo pia walichagulowa wenyeviti wa Kamati ambapo Musa Gama alitetea nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Leon Lucas akichaguliwa Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mwanamkasi Madega akichaguliwa Kamati ya Maadili.


Akizungumza baada ya uchaguzi huo Makamu Mwenyekiti Mkufya ameshukuru Madiwani kwa kuendelea kumuamini na kumchagua katika nafasi hiyo


Mkufya amesema ataendeleza ushirikiano wa awali kati yake Madiwani na Viongozi wa Serikali katika kuhakikisha malengo ya maendeleo yanapatikana.


Amesema atahakikisha malengo ya makusanyo ya ndani yanafikiwa kwa ushirikiano wa Madiwani na Watendaji Ili fedha hizo zitekeleze miradi ya maendeleo na kuondoa vikwazo kwa wananchi.


Mwisho

No comments: