WANANCHI KIJIJI CHA SANGAIWE WAJENGA SHULE YA MSINGI KWA THAMANI YA MILLIONI 300 KUSAIDIA WANAFUNZI KUTOTEMBEA KILOMITA TISA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 11 August 2024

WANANCHI KIJIJI CHA SANGAIWE WAJENGA SHULE YA MSINGI KWA THAMANI YA MILLIONI 300 KUSAIDIA WANAFUNZI KUTOTEMBEA KILOMITA TISA

Jiwe la uzinduzi wa shule ya Msingi Burunge

 
Muonekano wa shule

 Epifania Magingo, babati


 Kutokana na adha ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu wa takribani kilomita 8 hadi 9 pamoja na kukabiliana na wanyama wakali pindi wanapoenda  shule , Serikali ya Kijiji Cha Sangaiwe Wilayani babati Mkoani Manyara imeamua kujenga Shule ya Msingi Burunge yenye thamani ya Shilingi milioni 338 ,637,300 ikiwa ni michango ya Wananchi na fedha za wawekezaji.

 Ujenzi wa Shule ya hiyo ulianza mwaka 2020 na kukamilika 2022 ambapo Wananchi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanyama Pori  (JUHIBU) walichanga fedha za ujenzi huo na August 9,2024 shule hiyo  ilizinduliwa yenye idadi ya wanafunzi 233 kuanzia Darasa la awali mpaka Darasa la Tano.

Pamoja na kufanikisha ujenzi wa Shule hiyo imeelezwa kuwa inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme,uhakika wa maji,uhaba wa walimu pamoja na miundombinu ya barabara inayoelekea kwenye Shule hiyo.

Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la uzinduzi wa  Shule ya Msingi Burunge katika Kijiji Cha Sangaiwe Mkuu wa Wilaya ya Babati Mji Lazaro Jacob Twange amewaasa Wananchi wa eneo hilo kutunza wawekezaji pamoja na kudumisha amani ili fedha zinazopatikana ziweze kujenga maendeleo na kuahudi kuwa kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika shule hiyo.

"Tunzeni ubia wenu na JUHIBU,Kuweni na mahusiaono mazuri na wawekezaji,shirikianeni na viongozi wenu, vurugu hazileti maendelo ,epukaneni na kesi za hovyo hovyo zinapunguza muda wa kufanya maendeleo,vurugu zinaleta chuki mtatumia pesa nyingi kwenda kwenye kesi haipendezi".

Amesema, Serikali pia itaendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo na kwamba walimu,wazazi na wanafunzi wanapaswa kushirikiana kuitunza shule hiyo ili iweze kuleta manufaa.

Aidha,Afisa Elimu kata ya Mwada Ester Kirway ametoa shukrani kwa uongozi wa serikali  ya Kijiji Cha Sangaiwe pamoja na Wananchi wa eneo hilo kwa kushirikiana pamoja ili kukamilisha ujenzi wa Shule ya Burunge.

"Sasa hivi tunajenga shule Kila kitongoji,na majengo baadhi yamekwisha Anza ,bado na malengo yetu baadae tunampango wa kujenga sekondari yetu sisi kama Kijiji Cha sangaiwe".

Kwa Upande wake Afisa Elimu wa Wilaya ya Babati Mji, Getrude Kavishe amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto waweze kuhudhuria shuleni kwakua shule hiyo  ipo karibu na makazi Yao tofauti na hapo awali na kusisitiza kuwa wazazi wanapaswa kuwa karibu na walimu ili kusaidia kupunguza utiro mashuleni.

"Niishukuru Serikali ya Sangaiwe kwa kazi nzuri ambayo wamefanya,watoto wetu watapata Elimu kwa karibu,naamin kwamba shule hii itakua Bora katika Halmashauri yetu ya Mji wa Babati ,ukaribu wetu wazazi na walimu utafanya wanafunzi waweze kufaulu vizuri".

Akisoma historia fupi ya Shule ya Msingi Burunge  Mtendaji wa Kijiji Cha Sangaiwe Amos Gurti Qares amesema ujenzi wa shule hiyo umegarimu kiasi Cha  Shilingi milioni 338,637,300 na inawalimu 3 wenye ajira ya kudumu na walimu 2 wameajiriwa na Serikali ya Kijiji. 

" Mgeni rasmi shule unayowekea jiwe la uzinduzi Leo inavyumba 7 vya Madarasa,ofis 3 za walimu,nyumba 2 za walimu,vyoo vya walimu matundu 2,vyoo vya wanafunzi matundu 10 na miundombinu yote imegharimu kiasi Cha shilingi million 338 ,mia 637 na Shilingi mia 300".

Imeelezwa kuwa hapo awali kabla ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Burunge watoto walikua wanatembea umbali wa kilomita 8 hadi 9 kwenda kosoma katika shule ya Msingi Sangaiwe jambo ambalo lilikua hatarishi kwa maisha ya wanafunzi hao.

 

No comments: