TWANGE AWATAKA VIJANA KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 11 August 2024

TWANGE AWATAKA VIJANA KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVU

 




Na Epifania Magingo, babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Wilaya ya Babati Mji Mkoani Manyara Lazaro Jacob Twange amewaasa vijana waliojitokeza kujiunga na mafunzo ya Jeshi la akiba kujiepusha na mienendo mibovu ikiwemo utumiaji wa vilevi  jambo ambalo litahatarisha afya zao. 


Mafunzo hayo yamelenga kuwafunza vijana ulinzi wa Taifa wakati wa amani na wakati wa vita na kulitumikia Taifa katika Hali mbalimbali hii inatokana na Sheria ya ulinzi wa Taifa.


Akizungumza wakati kufungua mafunzo ya Jeshi la akiba katika kata ya Mwada Wilayani babati Mkuu wa Wilaya ya Babati Mji Lazaro Jacob Twange amesema vijana hao wanapaswa kuwa na nidhamu kwakua ni msingi mzuri ambao utasidia kutimiza malengo yao.


" Jeshi msingi wake mkubwa ni nidhamu,Jeshi ambalo halina nidhamu limepotea,sikilizeni viongozi wenu,jitunzeni,acheni kunywa pombe Kali,acheni kuvuta bangi,jiepusheni na migogoro ,muwe chachu kwa kutoa msaada kwa jamii".


Amesema,elimu watakayoipata kupitia mafunzo hayo wanapaswa kutumia vizuri kwa kusaidia viongozi waliopo katika maeneo husika wanayoishi ili kukuza maendeleo ya Taifa.


" Wasaidieni viongozi wenu kaeni nao karibu ili kutatua migogoro,muwe chachu ya maendelo,nyinyi tayari mmeingia kwenye mtandao wa Serikali ,endeleeni kusoma vizuri na muheshimu ratiba."


Naye,Diwani wa kata ya Mwada Michael Mombo amesema usalama ukiwepo maendeleo yanapatikana kwa haraka na kwamba Wananchi wa  vijijini vya kata hiyo wamekubali wanafunzi hao wanunuliwe Sare za mafunzo.


" sisi kata ya Mwada tumekubali mafunzo haya wanakijiji wamekubali wanafunzi hawa wanunuliwe Sare zao,muheshimiwa Mkuu wa Wilaya utaona namna gani Wananchi hawa wameona hili ni Jeshi lao".

 

Mafunzo hayo yenye washiriki 360 ambapo wanawake ni 47  na wanaume 313 katika makundi mbalimbali  yalianza rasmi 18 June  2024 na kutarajiwa kukamilika 20 September 2024.

No comments: