NJOONI NANE NANE MJIFUNZE - RC BABU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 4 August 2024

NJOONI NANE NANE MJIFUNZE - RC BABU

 



Na Mwandishi wetu, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 


MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wakazi wa mikoa ya kanda ya Kaskazini kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho ya 30 ya kilimo ya nane nane yanayofanyika viwanja vya Themi Njiro jijini Arusha ili kujifunza mambo mbalimbali.


Babu ambaye pia ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha, amesema maonyesho hayo yana manufaa makubwa kwa wakulima kwani elimu ya kilimo, mifugo na uvuvi inatolewa kwa washiriki.


"Maonyesho haya yanashirikisha mikoa mitatu ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, hivyo watu washiriki kwa wingi kwani yamefunguliwa rasmi Agosti 3 na kufungwa Agosti 8," amesema Babu.


Amesema wakulima wakishiriki maonyesho hayo wanajifunza mambo mengi kupitia mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi yaliyopo.


"Washiriki watauliza maswali kwa wataalamu wetu wa kilimo, mifugo na uvuvi na kujionea kwa macho kupitia maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku nane," amesema Babu.


Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Raphael Lulandala ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amesema elimu inayotolewa kwenye maonyesho hayo ina tija kwani 


"Elimu ya ukulima na ufugaji ikitolewa ipasavyo matokeo chanya yatazidi kupatikana  kwenye jamii yetu hivyo washiriki kuja kujifunza ili wazalishe kwa ubora," amesema Lulandala.


Mmoja kati ya wakulima wa kanda ya Kaskazini Mwinyijuma Ismail kutoka kata ya Lengatei wilayani Kiteto ambaye ameshiriki maonyesha haya amesema amenifaika kwa kupata elimu ya ukulima na ufugaji wa kitaalamu.


Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu wa 2024 ni chagua viongozi wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi


MWISHO

No comments: