POLISI PWANI YAWASAKA MARAFIKI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA FUNDI UJENZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 19 August 2024

POLISI PWANI YAWASAKA MARAFIKI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA FUNDI UJENZI








Na Mwandishi wetu, MAIPAC KIBAHA


maipacarusha20@gmail.com


JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawasaka watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Ally Pweku (24) fundi ujenzi mkazi wa Mbwate Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema Agosti 18 mwaka huu Jeshi hilo lilipokea taarifa ya kupatikana kwa mwili wa marehemu huyo ukiwa umetelekezwa vichakani.


Kwa mujibu wa Kamanda Lutumo Agosti 12 mwaka huu marehemu alikuwa katika baa maarufu kwa jina la Tarimo iliyopo mtaa wa Msangani akiwa na rafiki zake wakipata vinywaji uliosababisha kupigana na baadae wote waliondoka kuelekea kusikojulikana.


Inasemekana baada ya kuondoka haikujulikana kilichoendelea hadi pale mwili wa marehemu ulipoonekana Agosti 18 akiwa amefariki na kutelekezwa kichakani.


Lutumo amesema kwasasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi wa daktari, huku Jeshi la Polisi likiendesha msako kuhakikisha wote waliohusika na mauaji wanatiwa mbaroni.


Polisi Mkoa wa Pwani wametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za waliohusika na mauaji hayo wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.


Mwisho

No comments: