RAIS SAMIA AMWAGIZA WAZIRINBASHE KUWEKA MIKAKATI KWENYE ZAO LA MBAAZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 3 August 2024

RAIS SAMIA AMWAGIZA WAZIRINBASHE KUWEKA MIKAKATI KWENYE ZAO LA MBAAZI

 

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan akizungumza na wakazi wa Gairo 

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan akikata utepe


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Gairo


Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan  amemwagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuweka mikakati itakayowezesha zao la mbaazi , kupata soko na bei nzuri kama ilivyo kwenye zao la korosho kwa ajlii kukuza kipato cha wakulima hao.


Pia aliwataka wananchi mkoani Morogoro kuhakikisha wanachagua viongozi bora katika uchaguzi mkuu wa Serikali za mitaa, watakaohamasisha maendeleo katika maeneo yao


Alisema hayo jana wilayani Gairo wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani  Morogoro ilioanza  wilayani  Gairo kwa lengo la kuangalia urejeshwaji wa miundombinu ilioharibiwa na mvua za  El nino.


"Natambua zao la mbaazi halina bei nzuri hapa ila limeni, limeni mazao ya chakula na biashara soko lipo, nimemwagiza waziri wa kilimo aweke mikakati ya zao hilo wilayani hapa,"alisema.


Aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanatimiza ahadi aliyotoa mbunge wao Ahamed Shabiby ya kutopoteza mtaa hata mmoja katika uchaguzi mkuu wa Serikali za mitaa mwaka huu.


"Mbunge wenu ameniahidi hapa kuwa hamtapoteza mtaa hata mmoja,  vilevile hakikisheni mnalinda na kudumisha amani na utulivu ili viongozi wenu wafanye kazi kwa utulivu.


"Nimekuja  kujionea mwenyewe matumizi ya fedha , nimeridhishwa miradi iliyotekelezwa, hospitali ya wilaya imejengwa vizuri" alisema.


Alisema kwa sasa changamoto ya maji Gairo inaenda kutatatuliwa baada ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi bilioni 34, na kwamba mikataba imeshasainiwa .


Vile vile alisema Gairo kulikuwa na changamoto ya kukatika umeme ambapo Serikali imejenga Substasheni  katika  wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambayo itatumika na wilaya ya Gairo.


"Gridi yetu ya Taifa ina umeme wa kutosha hivyo kujengwa kwa substasheni hiyo kutasaidia kupooza umeme na kuleta Gairo" alisema.


Hata hivyo alisema changamoto zote zinazowakabili wananchi wa Gairo zitatatuliwa na kwamba kila waziri atahakiksha anatatua Katika eneo lake.


Awali mbunge wa jimbo la Gairo Ahmed Shabiby alisema Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo makubwa katika kipindi cha miaka mitatu ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo haikuwepo hapo awali.


Alisema Serikali iliahidi kituo cha Afya cha Nongwe,  Magereza  na Mahakama  zote  zimekamelika na zinafanya kazi.


Pia ahadi ya  madaraja  mawili moja lenye urefu wa mita 80, na lingine urefu wa mita 100 ambayo yanauwezo wa kupita magari mawili, ambayo yanaunganisha  na barabara ya lami ya kwenda Kilindi.


Alisema barabara zote za Gairo zinapitika na kwamba hadi milimani kuna mawasiano ya simu na  miundombinu ya barabara..


Hata hivyo alisema Serikali ilitoa zaidi ya bilioni 18 kwaajili ya miradi ya elimu na Afya huku akiomba Serikali kuwaongezea idadi ya dawa kutokana na unyeti wa eneo hilo  ambalo linalohudumia   wananchi wa Kiteto na Kulindi.


Pia aliomba kuongezewa gari la wagonjwa kutokana na wilaya hiyo kupokea majeruhi wengi wa ajali za barabarani  mbali na wananchi wa Gairo.


Aidha aliomba Serikali kuwapatia ruzuku ya  mbegu za Alizeti  kwa wananchi wake sambamba na  soko la kisasa na stedi wilayani humo.


Kwa upande wake Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI  Mohamed Mchengerwa , alisema  katika kipindi cha miaka mitatu na  nusu ya Rais Samia mambo makubwa ya kizalendo yamefanyika ambayo yamegusa maisha ya Watanzania wa hali ya chini.


Alisema kwa wilaya ya Gairo zahanati 32 zimejengwa sambamba na hospitali ya wilaya pamoja na shule za sekondari na msingi lengo lilikuwa kusogeza huduma karibu na wananchi.


Baadhi ya wananchi waliozungumza na Maipac Media Tanzania kwa ujio wa Rais Samia walisema, kufika kwake mkoani hapa kutaongeza ufanisi kwa viongozi kufanya kazi, pamoja na kufungua fursa zaidi za kiuchumi.


Nassoro Rashid mkazi wa Gairo alisema Wilaya yao ni ya Kilimo muda wote na kwa kauli ya Rais kwa Waziri wa Kilimo kutafungua fursa ya kibiashara  na wafanyabiashara kuanza kuwatambua na kuwathamini wakulima.


Mwisho.

No comments: