PROF. MKENDA AZINDUA BODI YA USHAURI ADEM - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 3 August 2024

PROF. MKENDA AZINDUA BODI YA USHAURI ADEM






NA: Julieth Mkireri, Maipac BAGAMOYO


maipacarusha20@gmail.com 


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu - Adem ambapo ametoa maelekezo kuhakikisha inafanya kazi Kwa kusimamia weledi na kuisaidia Serikali.


Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyoProf Mkenda amewahimiza Wajumbe kwenda kuwasaidia Walimu wanaofundisha kwenda kujiendeleza katika Elimu.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM Maulid Maulid amesema kuwa watahakikisha wanasimamia maelekezo yote waliyopewa na kuishauri Serikali kwa weledi Mkubwa.


Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt Leonard Akwilapo amesema kwa niaba ya Bodi watazingatia miongozo na kanunu za Sheria Katika kuongoza Bodi hiyo.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Carolyne Nombo amesema Bodi hiyo kama Serikali wanaimani nayo itafanya kazi Kwa weledi .


Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM Dkt Sixton Masanja amesema wamekuwa na Mafanikio makubwa ya ongezeko la wanafunzi ambao wamepita hapo pamoja na kuongeza uwezo wa ufanyaji kazi Kwa watumishi.


Mwisho

No comments: