RAIS SAMIA AWAALIKA WAWEKEZAJI KILOMBERO, MALINYI NA ULANGA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 6 August 2024

RAIS SAMIA AWAALIKA WAWEKEZAJI KILOMBERO, MALINYI NA ULANGA

 

RAIS SAMIA akiwahutubia wakazi wa Ifakara wakati alihitimisha Ziara yake Mkoani Morogoro 






📌 *Ni kutokana na uwepo wa umeme wa kutosha katika kituo cha umeme Ifakara* 


📌 *Asema Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa umeme wa kutosha*


📌 *Vijiji vyote 110  Wilaya ya Kilombero vyafikiwa na umeme*


Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji uwepo wa umeme wa uhakika katika Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga na hivyo amewaalika kwenda kuwekeza katika maeneo hayo.


Rais Samia  aliyasema hayo Agosti 05, 2024 wakati akihitimisha ziara yake katika Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambapo amesisitiza  kuwa uongezaji thamani wa bidhaa katika viwanda unahitaji uwepo wa umeme wa uhakika hivyo Serikali inafanya kila jitihada ili nchi iweze kujitosheleza na nishati hiyo na kuwezesha uongezaji thamani malighafi zinazopatikana nchini ikiwemo mazao.


Aliwahakikishia wawekezaji kuwa, maeneo ya Kilombero, Malinyi na Ulanga yatakuwa na umeme wa kutosha hivyo  wawekezaji wasisite kuendelea kuwekeza katika viwanda mbalimbali.


Aliongeza kuwa, kupatikana kwa umeme katika maeneo hayo kumeendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani ambao wameweka mashine za kuchakata nafaka na kuongeza kuwa ujenzi mkubwa wa maghala unaendelea. 


"Uwekezaji huu unaonesha  kwamba umeme umeleta faida kubwa ndani ya maeneo haya, niwahakikishie Serikali itaendelea kusimamia Sekta ya Nishati ili  kuendelea kuwa na umeme wa uhakika."alisisitiza Rais Samia


Akizungumzia miradi ya umeme vijijini, alisema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeshapeleka umeme kwenye vijiji vyote 110 vya Wilaya ya Kilombero. 


Ameongeza kuwa kazi inayoendelea sasa ni upelekaji wa umeme kwenye Vitongoji na kwenye Taasisi.


....

No comments: