Wakandarasi Wazawa washinda zabuni ya Bilion 5 Mkoani MANYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 5 August 2024

Wakandarasi Wazawa washinda zabuni ya Bilion 5 Mkoani MANYARA

 




Na Epifania Magingo,babati


maipacarusha20@gmail.com 


Wakandarasi wazawa hapa nchini wanakumbwa na changamoto ya kutolipwa fedha  kwa wakati na Serikali pindi wanapoingia mikataba ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kufanya kuwa na ugumu wa kumaliza tenda hizo kwa wakati.


Hayo yamejiri wakati wa hafla fupi ya usainishwaji wa mikataba 17 ya awali Mkoani Manyara kwa baadhi ya Wakandarasi wazawa hapa nchini ambao   wameshinda zabuni yenye thamani ya Shilingi Billion 5.2  kwaajili ya kushughulikia miundombinu ya barabara za mjini na vijijini Mkoani Manyara Chini ya usimamizi wa  wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA. 


Akizingumza wakati wa hafla hiyo Mhandisi Anna Sanga ameiyomba Serikali kuwaangalia wakandarasi hao kwa jicho la kipekee ili kukamilisha malipo Yao na kazi ziweze kuisha kwa wakati.


Hata hivyo,Amesema,pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakandarasi hao ameahidi kwamba kwa tenda mpya  ambayo  wamesaini watahakikisha inafanyiwa kazi kwa wakati na viwango vinavyohitajika. 


"Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kufanya kazi kwa wakati na kwa viwango vilivyooanishwa katika mikataba yetu".


Kutokana na changamoto hiyo ya madai ya wakandarasi hao Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameahidi kwamba malalamiko hayo atashughulikia  ndani ya Muda mfupi na fedha hizo zitalipwa na kuwataka wakandarasi hao kufanya kazi kwa weledi na kutokwamisha mradi huo mpya ambao wameingia mkataba.


Amesema,wakandarasi wanapaswa kuwaajiri vibarua wananchi waliopo eneo husika ili na wao waweze kunufaika na mradi huo wa maendeleo na kwamba fedha hizo za malipo zinatokana na Kodi za wananchi.


" Fedha mnazolipwa ni Kodi za Wananchi,tambueni mzigo mlionao ni mkubwa,hivyo fanyeni kazi kwa weledi Kila fedha mtakayoiona iwaume roho kwakua ni fedha za walipa Kodi na imerudi kufanya kazi mbalimbali za jamii".


"Mikataba hiyo yote Leo imesajniwa na wazalendo kwaio kazi kubwa ambayo inafanywa ni utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi" kati ya miongozo ni kuboresha miundombinu ya barabara mjini na vijijini."


Qeen Sendiga ametoa msisitizo kwa wakandarasi wa mradi huo kwamba wakati wa kutekeleza mradi wazingatie kusimamia majukumu kikamilifu ili kuondokana na uharibifu wa  miundombinu katika eneo husika.


"Miradi inapoenda kutekelezwa kwenye maeneo lazima ilete faida,mashimo yanayochimbwa baada ya mradi tuangalie namna ya kuyaacha ili yawe  faida ingaliwe namna yanaweza kuwa mabwawa ya kunyweshea maji mifugo".


Aidha,kiongozi huyo ametoa angalizo kwa wakandarasi hao kuwa wakati wa ukaguzi wa mradi huo wanapaswa kuwepo eneo la tukio  na kuwasisitiza kazi ifanyike kwa Muda uliopangwa ili kuepusha uwepo wa viporo kwenye miradi.


"Mkandarasi niliekupa kazi nikipita kwenye mradi sijakukuta ujue kwamba kazi zijazo sitasaini mkataba wako,sijampa kazi fundi wako ,nataka maswali nitakayouliza mkandarasi aweze kunijibu na sio fundi".


Meneja wa TARURA Mkoa wa Manyara Salimu Bwaya amesema watajipanga  kuhakikisha miradi inasimamiwa vizuri ili kuleta manufaa kwa wananchi.


" Niwahakikishie ushirikiano utatolewa wa Hali ya juu ila kazi ifanyike kwa ufanisi na kwa wakati".


Amesema,amepipogeza Serikali kwa kutoa kazi hiyo kwa wakandarasi wazawa kwakua itaendelea kuwajengea uwezo na ufanisi mkubwa katika utendaji kazi kwa lengo la kuboresha maendeleo ya nchi.

No comments: