RC Sendiga Apanda Miti 1500 Eneo La Mradi Hanang' - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 13 August 2024

RC Sendiga Apanda Miti 1500 Eneo La Mradi Hanang'

 





Na Epifania Magingo, babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga ameongoza zoezi la upandaji miti takribani 1500 Wilayani Hanang kwenye eneo ambalo Serikali imejenga nyumba za mradi  kwa ajili ya kuwapatia wahanga  wa maafa  ya maporomoko ya tope  mlima Hanang yaliyotokea 3 December  2023. 


Miti hiyo iliyopandwa ni mchanganyiko mbalimbali ikiwemo miti ya matunda ambayo imetolewa na Mbunge wa Vijana Taifa Asia Halamga.


Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji miti hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga ametoa maagizo kwa uongozi wa Wilaya ya Hanang kuhakikisha wanaweka alama na maelekezo ya makatazo ya kutaka  mifugo haikatizi kwenye maeneo hayo  kwakua itaharibu mazingira.


"Jukumu la kuhakikisha kwamba hapa mifugo haipiti ni la Wilaya,kuanzia kule Chini wekeni vibao wanaopita wawe wanasoma,msipitishe mifugo eneo hili lakin pia Mkurugenzi muweke visheria vyenu vile vya Halamshauri , atakae kaidi atakutana na Sheria huzi".


Aidha, shuhuli ya umwagiliaji wa miti hiyo imekabidhiwa kwa Jeshi la Magereza  ili kuhakikisha kwamba inakua na uangalizi mzuri pamoja na kuzaa matunda kwa ile ya matunda.


"Mkurugenzi na timu Yako mtengeneze utaratibu mzuri  wa upatikanaji wa maji lakini pia mkae na kamanda wa gereza badala ya kutafuta vibarua wenyeji ambao wanakuja hawaji bora kuchukua hapa ambao tunauhakika nao".


Mbunge wa Vijana Taifa Asia Halamga amesema ameamua kuchukua jukumu kama kijana kwa kushirikiana na Vijana wengine kwa kupanda miti ikiwa ni mwendelezo wa kufuata agizo la Serikali katika suala la kutunza mazingira.


"Muheshimiwa rais ametoa fedha nyingi sana tunamshukuru kwa kuwajengea ndugu zetu ambao walipata shida kubwa  katika kipindi kile Cha mafuriko,sisi kama Vijana kupitia mbunge wao Vijana nikasema na sisi tufanye kitu,tukasema tutaleta miti ili kuunga mkono Serikali na siku ya Leo tumepanda miti 1500".


Ikumbukwe kuwa maporomoko ya tope mlima Hanang yalitokea 3 December mwaka 2023 kata ya mogito Wilayani Hanang Mkoani Manyara na kusababisha vifo vya watu  89 na majeruhi 139.

No comments: