Utalii na Michezo ni Chachu ya Uchumi Mkoa wa MANYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 13 August 2024

Utalii na Michezo ni Chachu ya Uchumi Mkoa wa MANYARA

 




Na Epifania Magingo, babati


maipacarusha20@gmail.com 


Baada ya mchezo wa mechi ya kirafiki kati ya Timu ya Fountaingate FC ya Mkoani Manyara pamoja na Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor mahia 2023/2024 uliopigwa katika uwanja wa Tanzanite kwaraa Babati Mjini Mkoani Manyara Klabu hizo zikashika njia na kufanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Wanyama Pori Tarangire iliopo Mkoani humo.


Mechi hiyo ilichezwa kwa lengo la kuikaribisha timu ya Fountaingate FC Mkoani Manyara kama timu rasmi ya Mkoa huo.


Akizungumza  wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga amesema kuna uwiano mkubwa  kati ya michezo na utalii kwakua kuna huduma nyingi ambazo zinapatikana.


"Tuliona jambo la hekima wageni wasiondoke bila kutembelea hifadhi zetu,tunajua utalii ndani yake kumebeba vitu vingi sana, kuna michezo, huduma na vitu kama hivo, lakini sisi tukaona tuunganishe utalii pamoja na michezo".


"Na kwakua mkoa wetu tunahifadhi mbili za kitaifa,tuna Tarangire na Manyara,tumeona tuwalete kwa Upande huu wa Tarangire kwasababu  ni hifadhi ya pili kwa kupokea wageni Tanzania ukitoka Serengeti National Park".


Queen Sendiga amesema kama Serikali wameona vyema  kuwapeleka wageni  kutembelea  mbuga ya Wanyama ili wageni waweze kuona ahasa kilichopo ndani ya nchi tofauti na michezo ikiwa ni kuonyesha msisitizo wa kuwa na utalii wa ndani kwa wazawa.


" Kwaio tunategemea hawa wote wakitoka huku  watakua mabalozi wazuri wa kutangaza nchi hapa pana timu ya Zaidi ya watu 80 amabo wote ni watu maarufu kulingana na kazi zao".


Aidha,amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya  mipango ili kuweza kuona ni kwa namna gani wachezaji wa timu ya fountaingate FC kuweza kuwa mabalozi wa kutangaza hifadhi hizo ndani ya Mkoa wa Manyara.


Amesema kwa timu zote ambazo zinakuja kucheza Mkoani Manyara wanapaswa kutenga Muda wa kwenda kutembelea hifadhi hizo baada ya mechi ili kusaidia kuitangaza nchi.


Naye,Meneja wa Timu ya Gor mahia ya Kenya amesema amefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kuweka uhusiano mzuri kati ya Serikali na sekta ya michezo katika kushughulikia michezo ikiwa pamoja na kupata fursa ya kutembelea hifadhi ya Tarangire.


" Ligi ya Tanzania Iko vizuri na inaipita yetu Kenya kwasababu gani Serikali ya Tanzania inauhusiano mzuri na matimu,inaudhamini wa kutosha mana ukiwa na udhamini mwingi na uhusiano mzuri timu inakua inanenepa."


"Aaah tarangire naeza sema hii ni mara yangu ya kwanza fika  na tumeshukuru sana kwa wadhamini na kamanda Rc kwa kuorganize kitu kama hiki,tunasema Asante sana kwa wandugu zetu wa Tanzania pia tuna wadhamini wetu ni mmoja tumeona Wanyama na tumefurai".

No comments: