RC SENDIGA AWAHIMIZA VIJANA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 29 August 2024

RC SENDIGA AWAHIMIZA VIJANA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga


Na: Epifania Magingo, Babati


maipacarusha20@gmail.com


Vijana wameaswa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika uboreshaji wa daftari la mpiga kura la Serikali  za Mitaa kwa ajili kuchagua Viongozi wa Serikali za Mtaa utakaofanyika Novemba 27,2024.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizungumzia maandalizi ya Uchaguzi huo Mjini Babati mbele ya waandishi wa Habari.


Amesema uandikishaji utaanza rasmi Septemba mosi mwaka huu ukiambatana na matembezi yatakayofanyika kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Manyara.


Qeen Sendiga amesema Vijana wanapaswa kugombea hasa Vijana  wanawake na kina mama  wajitokeze kwa wingi kwakua watawakilisha sauti ya mama kuanzia  ngazi ya chini.


"wito wangu kwa Vijana nendeeni mkagombee,hesabu inaanza na Moja,kama unajiona wewe unasifa jitokeze,lakini sana wakina mama mkagombee,tunachangamoto sana kwenye Mkoa wetu katika lisha na ukatili,lakini tukiwa na kina mama wengi itanisaidia katika kupanga maendeleo".


Aidha, amesema ili kuhamasisha zoezi hilo la kujiandikisha Serikali ya Mkoa imeàmua kutumia michezo kwaajili ya kuunganisha Serikali na jamii ambapo Wananchi watakimbia au kutembea kilomita nane kwa mzunguko mzima pia itasaidia kuimarisha afya.

 

"Kwenye michezo tunauhakika tutakamata watu wa rika zote,maana michezo pia inahamasisha afya, michezo pia ni kiungo muhimu sana Cha upashanaji habari kwaio ni muhimu sana". Alisema


Amesema Kila mtanzania anahaki ya kujiandikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura la Serikali za Mitaa pamoja na kugombea kwenye nafasi za uongozi kuanzia Serikali za Mitaa hadi ngazi za juu.


Nao, baadhi ya Vijana Mkoani Manyara  akiwemo Lucas Alphonce amesema Vijana wanapaswa kuamka na kugombea katika nafasi mbalimbali ili kuleta hamasa ya maendeleo kwa Taifa huku Elisha Ako mazazi wa Hanang amewshauri Vijana wenye vigezo vya kugombea katika nafasi mbalimbali wagombee kwa wingi.

No comments: