Tanga wataka wajengewa reli ya SGR - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 29 August 2024

Tanga wataka wajengewa reli ya SGR

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dr Batilda Buriani




Burhani Yakub,Tanga.

Wakazi wa Mkoa wa Tanga,wamependekeza kujengwa kwa reli ya kisasa ya umeme ya SGR kutoka jijini Tanga yenye kuunganishwa na mikoa ya kanda ya Kaskazini na ile ya sasa iwe miongoni mwa miradi ya kimkakati itakayoingizwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050.

Wamesema Reli hiyo itarahisisha na kuongeza kasi ya usafirishaji wa shehena kutoka bandari ya Tanga ambayo imeanza kupokea meli kubwa kutoka nchi mbalimbali Duniani baada ya kuchimbwa kina na kupanuliwa.

Wametoa mapendekezo hayo wakati wa kikao kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dr Batilda Buriani cha kupokea na kujadili taarifa ya maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 hadi 2050 kutoka Wilaya nane za mkoani hapa.

Mbunge wa zamani wa jimbo la Tanga, Mussa Mbarouk amesema uboreshaji wa bandari ya Tanga ni vyema uende sambamba na ujenzi wa reli ya SGR kutoka bandari ya Tanga itakayounganishwa na nchi za maziwa makuu.

“Katika kipindi hiki cha 2025 hadi 2050 mipango ya ujenzi wa reli ya SGR iingizwe kwenye dira ya maendeleo ili uongozi wowote utakaokuwa madarakani uwe kupata urahisi wa kutekeleza..itasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya mikoa ya akanda ya kaskazini,Tanzania na nchi za maziwa makuu kwani shehena na mazao ya wakulima yatasafirishwa kwa urahisi kuliko ilivyo sasa”amesema Mbarouk.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema ametaja maeneo yalaiyojitokeza wakati wa kuchangia dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025-2050 katika Wilaya za mkoa wa Tanga kuwa ni pamoja na suala zima na mapinduzi ya kiuchumi, maendeleo ya watu na jamaii, utawala bora, haki, ulinzi na usalama.

Maeneo mengine ni maendeleo ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi,  mazingira ana mabadiliko ya tabianchi, ustawi wa wazee na makundi maalumu na suala zima la kuongeza wigo wa sifa za kujiunga na jeshi la kujenga Taifa.

No comments: