TAKUKURU yabaini miradi ya sh 1.1 Bilioni kuwa na mapungufu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 2 August 2024

TAKUKURU yabaini miradi ya sh 1.1 Bilioni kuwa na mapungufu





Na: Burhani Yakub Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeanza kuchunguza miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya sh 1.1.bilion iiliyobainikanika kuwa na mapungufu wakati wa utekelezaji.


Miradi hiyo ni kati ya 79 yenye thamani ya sh 34.5 bilioni iliyotekelezwa katika sekta za kipaumbele ambazo ni elimu, barabara, maji na Afya.


Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru mkoa wa Tanga, Frank Mapunda (pichani) wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni mwaka 2024 .


Ametaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Kisinga wenye thamani ya sh 50 milioni katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, ujenzi wa zahanati ya Milingano wenye thamani ya sh 553, milioni, upanuzi wa kituo cha Afya Mgwashi wenye thamani ya sh 500, milioni na mradi wa zahanati ya Mkaalie wenye thamani ya sh 50 milioni.


Amesema katika utekelezaji wa jukumu la uelimishaji jamii, Takukuru imewafikia wananchi 643,548 kupitia mikutano ya hadhara 37 na maonesho 10 huku ikiwafikia wanafunzi wa shule na vyuo 38,751 kupitia uimarishaji wa klabu 71 za wapigakura.


Kuhusu taarifa amesema Takukuru imepokea taarifa 111 ambapo taarifa 66 zilihusu vitendo vya rushwa na taarifa 45 hazikuhusu vitendo vya rushwa huku ikifungua mashauri Saba mahakamani ambayo Jamhuri imeshinda mashauri sita na jumla ya mashauri 70 yakiwa yanaendelea katika mahakama mbalimbali mkoani Tanga.

MWISHO

No comments: