TUGHE MANYARA YAWATAKA WAAJIRI KUZINGATIA KIKOKOTOO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 20 August 2024

TUGHE MANYARA YAWATAKA WAAJIRI KUZINGATIA KIKOKOTOO

 




Na Epifania Magingo, Babati,


maipacarusha20@gmail.com 


Serikali imeombwa kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu wafanyakazi ikiwemo kushughulikia suala la waajiri  kuwacheleweshea  mishahara  wafanyakazi wao jambo ambalo linapunguza Kasi ya kufanya kazi.

  

Ombi Hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha  wafanyakazi wa Serikali na Afya Mkoa wa Manyara (TUGHE) Honest Temba  katika kikao Cha utolewaji wa taarifa ya utekelezaji wa Chama  kuanzia October 2021 Hadi Julai 2024.


Amesema,waajiri wengi pia hawazingatii kikokotoo ambacho kimeanzishwa kwa wafanyakazi hao jambo ambalo limeleta sintofamu kwa watumishi.


"Changamoto ambayo wanakabiliwa nayo wafanyakazi hasa kwa waajiri wao sana sana ni suala la hiki kikokotoo ambacho kimeanzishwa Hilo ndo changamoto kubwa ambalo tumelizungumzia na tunazidi kuiomba serikali kuliangalia upya na uganyike uwezekano wa kurekibisha".


Amesema,TUGHE imeona umuhimu wa kuhamasisha kwa uundwaji wa mabaraza ya wafanyakazi kwenye maeneo Yao ya kazi ili kusaidia kujadili changamoto mbalimbali wanazozipata wafanyakazi.


Aidha,Katibu wa TUGHE  Mkoa wa Manyara Tamsoni Mshighati amesemà chama hicho kimekua na mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia changamoto za wafanyaki na kuhakikisha wafanyakazi wanakua salama na kulinda ajira zao.


"Wapo watumishi wengi ambao walipata kesi,na wengine ni za jinai lakini zingine hazina ukweli ndani yake,na kwa mujibu wa Sheria lazima mahakama iseme kwamba uyu ametenda kosa huyu hajatenda, lakini TUGHE imekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea ,kuwasimamia,katika vyombo vya kisheria na kuhakikisha wanakua salama na ajira zao zinalindwa".


Amesema,lengo la chama hicho ni kuhakikisha kwamba wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi wanafurahia kazi yao kwasababu mudà mwingi wa wafanyakazi wanautumia wakiwa maeno ya kazi tofauti wakiwa majumbani kwao.


"Kwaio lazima tuhakikishe kwamba maeno ya kazi yanakua salama wanafurahia maeneo ya kazi,wanapata kile ambacho Sheria imeelekeza kwaajili ya mustakabali wa ajira yao lakini pia kwaajili ya mustakabali wa taasisi".


Amesema,pamoja na mafanikio kadhaa yaliyopatikana ndani ya chama hicho,matarajio Yao ni kwamba chama kinafanya jitihada za kuongeza wanachama wengine na wao waweze kunufaika.


Nao,baadhi ya wanachama wa TUGHE idara ya afya Mkoani Manyara wamezungumzia umuhimu wa kujiunga na chama hicho pamoja na changamoto zinazowakumba wafanyakazi hao.


Naye,Mwenyekiti wa TUGHE wanawake Mkoa wa Manyara Judith Mwambola ametoa rai kwa wafanyakazi wengine kujiunga na chama hicho kwakua kitamsaidia kupata haki zake pindi atakapokutwa na matatizo.


"Mfano Mimi silipwi stahiki zangu lakini naogopa kumfata mwajiri wangu lakini nikienda kwa katibu ambae ndo mwanasheria anaweza kunisaidia na matatizo yangu yakaisha.


Amesema, Serikali pia inaombwa kuyatazama mabaraza ya wafanyakazi yaliyopo mahali pa kazi kwakua huko ndipo kunapoibuliwa changamoto za wafanyakazi ili ziweze kutatuliwa.


" Lakini mabaraza ya wafanyakazi hua mengine yanafanyika, sehemu zingine hazifanyiki na hichi ni kilio Cha Taifa,kuna Wilaya zingine hazifanyi,kwaio tunaomba Serikali hili walitazame".

No comments: