UBORESHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA MARA, SIMIYU NA MANYARA KUANZA SEPT 4-10,2024 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 25 August 2024

UBORESHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA MARA, SIMIYU NA MANYARA KUANZA SEPT 4-10,2024

 




Na Mwandishi Wetu, maipac 


maipacarusha20@gmail.com 



Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Mara, Simiyu na Wilaya tatu za Babati, Hanang na Mbulu Mkoa wa Manyara kuanza Septemba 4-10/2024.


Mwenyekiti Tume Huru ya Taifa  Jaji Jacobs Mwambegele akifungua Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura leo Jumapili agosti 25, 2024 mjini Musoma amesema, huo utakuwa ni mzunguko wa nne wa uboreshaji daftari hilo.


Amesema, Tume imeweka utaratibu kwa watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito na akina mama wenye watoto wanafunga wachanga watakao kwenda nao vituoni.


Kuhusu wenye kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni halali na zitatumika kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 168 cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Namba 1 ya mwaka 2024.


Ametoa tahadhari watu kujiepusha kujiandikisha kuwa mpiga kura zaidi ya mara moja ni kosa la Kisheria kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 1 ya mwaka 2024, akitiwa hatiani adhabu ni faini isiyopungua sh100,000 na isiyozidi 300,000 au kifungo kisichopungia miezi 6 na kizichozidi miaka miwili au vyote pamoja.


Mkutano huo unahusisha viongozi wa vyama vya kisiasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa wenye ulemavu, wazee wa mila, vyombo vya ulinzi, asasi za kiraia, watendaji wa tume, waandishi wa habari na wawakilishi wa wanawake.

No comments: