WAKULIMA WA MAHINDI BABATI WAWALALAMIKIA NFRA KUCHELEWESHA MALIPO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 31 August 2024

WAKULIMA WA MAHINDI BABATI WAWALALAMIKIA NFRA KUCHELEWESHA MALIPO

 



Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Wakulima wa zao la mahindi Wilayani Babati Mkoani Manyara wamelalamikia  kucheleweshwa malipo ya mazao waliyouza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) tawi la Babati na kuiyomba Serikali ishughulikie changamoto hiuo ili waweze kulipwa kwa wakati.


Wakitoa malalamiko yao mbele ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Hussein Mohammed ambaye amefanya ziara yake kwenye Mkoa wa Manyara na kukagua shughuli za NFRA Wilayani Babati, mmoja kati ya wakulima hao Ally Said amesema wanapofanya biashara pesa inatakiwa itolewe kwa wakati ili waweze kunufaika.


"Changamoto kubwa kama unavoona hapa watuwaishie tu malipo yetu tuendelee na mchakato wa kazi ili na sisi tuweze kununua mahitaji mengine,kama unavoona hapa magari hamna yanakuja yanashusha mzigo na kuondoka".


Baada ya kupokea malalamiko hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Hussein Mohammed ametoa maelekezo ya Serikali na kumtaka Mkurugenzi wa NFRA kuwalipa wakulima hao ndani ya siku tatu.


"Maagizo ya Wizara ya kilimo kwa Mkurugenzi wa NFRA ahakikishe kwamba malipo ya watu wote waliouzia mazao NFRA yasizidi Zaidi ya siku tatu mwananchi awe amelipwa haki zake.


Aidha,amesema muitikio mkubwa wa Wakulima uliopo kwa sasa  kujikita Katika suala la kilimo ndio mkombozi wa Taifa kwenye Upande wa chakula na kwamba Kila mwananchi anapaswa kuunga juhudi za Serikali.


Naibu Katibu Mkuu Hussein ametoa msisitizo kwa wakulima kuwa waendelee kupeleka mazao yao NFRA kwakua changamoto zilizopo katika vituo hivyo zimeanzwa kufanyiwa kazi.


Naye,Msimamizi Mkuu wa Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA)Tawi la Babati amesema watatekekeza maelekezo ya Serikali mara Moja kama ilivoagizwa huku akiwashauri wakulima kuwa makini kwa kuzingatia mahindi yamekauka vizuri ili kukidhi vigezo ili zao hilo like siweze kukataliwa.


"Njia rahisi ya kukagua mahindi kama yamekauka vizuri au bado unachukua kopo la maji unayatia mahindi unachanganya na chumi unatikisa kopo kwa dakika tatu ukiyaancha baada ya mda na ukikuta yanaunyevu unyevu utagundua hayajakauka vizuri".


Hata hivyo,amesema wakulima wanapaswa kuchangamkia fursa ya kuwauzia mazoa yao NFRA kwakua yatanunuliwa kwa bei rafiki ambayo Kila mkulima atapata manufaa.

No comments: