WATALII 1,000 WATEMBELEA HIFADHI MIKUMI KWA WAKATI MMOJA,NI WALIMU WA JIJI LA DAR - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 4 August 2024

WATALII 1,000 WATEMBELEA HIFADHI MIKUMI KWA WAKATI MMOJA,NI WALIMU WA JIJI LA DAR






Na: Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


HIFADHI ya Taifa ya Mikumi iliyopo Wilaya ya Kilosa kwa wakati mmoja imepokea watalii 1,000 kutoka jijini Dar es salaam ambao ni walimu wa shule mbalimbali kutoka jijini humo.

Uongozi wa Hifadhi ya Taifa Mikumi umesema kutokana na kupokea watalii hao, uko tayari kuwapokea watalii na wageni wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Kaimu mkuu wa Hifadhi hiyo Helman Mtei alisema hayo baada ya kupokea watalii wa ndani zaidi Ya 1000 kutoka mkoani Dar es salaam. 

Mtei ambaye ni Afisa mwandamizi wa Hifadhi ya Mikumi alisema kutokana na kuanza kwa treni ya SGR wanatarajia kupata wageni wengi zaidi ambao watatembelea hifadhi hiyo.

"Tumejiandaa na tuko tayari kupokea idadi yoyote ya wageni na tutawahudumia vizuri kwa chakula, malazi na utalii wa Kuona wanyama hifadhini" alisema Mtei.

Aliongeza kuwa  serikali imeboresha miundombinu ya usafiri kwa kufungua reli ya SGR na kufanya Mikumi ifikike haraka zaidi kwa sasa.

"Kwa msaada wa SGR Mikumi Sasa inafikika haraka hivyo na jukumu letu watumishi kuwa wabunifu Ili kusaidia kufikiwa lengo la serikali la kupokea watalii milioni Tano Kwa mwaka" alisema Mtei 

Katibu Tawala mkoa wa Dar es salaam Dk Toba Nguvila aliyeongoza msafara wa walimu alisema tren ya SGR imepunguza gharama za usafiri.

"Watu wengi walishindwa kufika MIKUMI kutokana na gharama za usafiri ikiwemo kutumia muda mrefu barabarani"alisema Dr Nguvila.

Alisema walimu hao kwa kushitikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa waliamua kutalii Hifadhi ya mikumi kwa kuafiri na SGR Ili kuwa mabarozi wa usafiri salama na haraka wa treni hiyo

Kwa upande wao walimu hao walisema pamoja na kufurahia usafiri huo ambao ni wa muda mfupi na hauchoshi walitaka kupumzika na kujifunza zaidi.

"Tumekuja kupumzika, kupunguza msongo wa mawazo na kujifunza kwa vitendo Yale tunawafundisha watoto" alisema mwalimu Hafsa Kileo.

Mwisho.

No comments: