Bega kwa Bega na mama Samia wachagia damu Tanga - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 24 September 2024

Bega kwa Bega na mama Samia wachagia damu Tanga

 





Na: Burhani Yakub, Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 



Mkoa wa Tanga umejipanga kuhakikisha unavuka malengo ya ujusanyaji wa damu ili upatikane zaidi ya asilimia 100.04 iliyokusanywa katika kipindi kuanzia Januari hadi Disemba cha mwaka 2023.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Ussi Khamis  ametoa ahadi hiyo leo wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu salama lililoratibiwa na Bega kwa Bega na mama Samia lililofanyika uwanja wa Ramole jijini Tanga.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Disemba  mwaka 2023 mkoa wa Tanga uliweza kuvuka lengo la ujusanyaji wa damu salama ambapo ulifikia asilimia 100.04  na hivyo kutosheleza mahitaji ya Hospitali na vituo vya Afya vilivyopo mkoani hapa na nyingine kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako kuna mahitaji makubwa.

Ussi ambaye pia ni mratibu wa huduma za maabara huduma za damu salama mkoa wa Tanga amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kujitooea damu kwa kuwa hakuna kiwanda cha kuzalisha damu Duniani bali ni sharti itoke kwa binadamu.

Mratibu wa Taasisi ya Bega kwa Bega na mama Samia,Luth Matelela amesema mkoa wa Tanga umejipanga katika kusaidia jamii zaidi na kwamba damu salama inasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wakiwamo wanawake wajawazito hasa wakati wa kujifungua.

"Tumepita Mikoa mbalimbali lakini Tanga mmejipanga vyema maana unapochangia damu umesaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wakiwamo wanawake wajawazito hasa wakati wa kujifungua"amesema Luth.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Jafary Kubecha amewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya ubakaji,unyanyasaji wa kijinsia na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa pamoja na kuwaathiri wahanga kisaikolojia pia vinaliletea sifa mbaya jiji la Tanga.

"Mkoa wa Tanga upo katika maeneo yanayoongoza nchini katika matukio ya matumizi,upitishaji dawa za kulevya,ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na hayo licha ya kuathiri kisaikolojia lakini unazotesha shughuli zabuzalishaji mali"amesema Kubecha.

Katika kongamano hilo,afisa kutoka Taasisi ya kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru), Frank Mapunda ametaja maeneo ambayo yanahesabika kuwa ni rushwa katika uchaguzi kuwa ni pamoja na wagombea kugawa fedha,chakula,fulana na kofia ikiwa ni sehemu ya kuwashawishi wapiga kura kumchagua.

"Takukuru imeshatoa elimu katika makundi mbalimbali wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa kufafanua maeneo ambayo yanahesabika kuwa ni rushwa katika uchaguzi na adhabu zitakazochukuliwa kwa watakaokiuka"amesema Mapunda.

      MWISHO

No comments: