BOMBA ZA UMWAGILIAJI SHAMBA LA ASA MSIMBA KILOSA YAUNGUA MOTO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 20 September 2024

BOMBA ZA UMWAGILIAJI SHAMBA LA ASA MSIMBA KILOSA YAUNGUA MOTO

 

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka




Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


MBAAZI katika shamba la wakala wa Mbegu(ASA) Msimba lililopo Wilaya ya Kilosa Mkaoni Morogoro zimenusurika kutetekea kwa moto  baada ya mtu asiyejulikana kuwasha moto kwenye shamba hilo na kuunguza miundombinu ya umwagiliaji  mabomba zaidi ya 15.


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka,akipokea taarifa ya kuingia kwa shamba hilo kutoka kwa meneja wa shamba Samson Moleli ambaye alisema moto huo ulianza Septemba 14 mwaka huu Kisha kuthibitiwa na Septemba 19 kuzuka tena kwa mara nyingine.


Mollel alisema licha ya  moto huo kuharibu miundombinu ya umwagiliaji lakini pia umechoma sehemu ndogo ya shamba la Mbegu za mbaazi ambazo zipo kwenye majaribio ya awali kabla ya kupelekwa  Kwa wananchi.


Alisema kwa sasa wamewekeza nguvu kwenye kuthibiti moto huo licha ya mara nyingi kuzuka majira ya usiku ambapo hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka baada ya kupata maelezo ,aliagiza vyombo vya usalama kuchunguza chanzo cha moto huo ambao umekua ukizuka kila mwaka katika shamba hilo hasa nyakati kama hizi za maandalizi ya msimu wa Kilimo.


"Uchunguzi ni muhimu kufanyika kwa sababa Sasa inajirudia na haya yamekuwa mazoea, na atakae bainika hatua za kisheria zichukuliwe haraka na hii itakuwa fundisho,"alisema Mkuu huyo wa Wilaya.


DC Shaka alisema  pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia hiyo ya kuchoma moto hovyo lakini  aliwataka ASA kuimarisha Ulinzi katika mashamba hayo.


Alisema mashamba ni tegemeo kubwa kwa Taifa katika uzalishaji mbegu za mazao mbalimbali.


Mwisho.

No comments: