WAKUU WA MIKOA, WILAYA WATAKIWA KUWASAKA WALIPO WATOTO WALEMAVU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations

Friday 20 September 2024

WAKUU WA MIKOA, WILAYA WATAKIWA KUWASAKA WALIPO WATOTO WALEMAVU

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa akisukuma kitimwendo Cha mtoto mwenye ulemavu

Na Woinde Shizza , ARUSHA 

maipacarusha20@gmail.com 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwatafuta popote walipo watoto wenye ulemavu ambao wamekuwa wakifichwa majumbani na wazazi ama walezi na kuwanyima haki ya elimu.

Mchengerwa ameyasema hayo  wakati akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya utekelezaji wa elimu Jumuishi , katika shule maalumu ya Sekondari Patandi wilayani Arumeru Mkoani Arusha ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa Salamanka uliosainiwa na serikali mwaka 1994 na kuanza kutumika rasmi mwaka 1997.

Alisema nchi yetu Tanzania elimu Jumuishi ilianza kutekelezwa muda mrefu kupitia sera ya elimu ya mwaka 1978 iliyoelekeza upatikanaji wa elimu kwa kila mtoto, utekelezaji wa sheria hiyo kwa watoto wenye mahitaji maalumu umerasimishwa mwaka 1998 kupitia mradi wa wizara ya elimu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la elimu , sayansi na utamaduni (UNESCO).

"Katika Taifa Letu bado tuna watu wenye kufikiri kwamba mtoto mwenye changamoto hana haki ya kupata elimu, nichukue nafasi hii kuwaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, wekeni utaratibu wa kufuatilia jamii hiyo kuanzia ngazi ya makazi ya wananchi kama kuna mtoto mwenye changamoto amefichwa serikali ichukue hatua mara moja"

Waziri amesema kuwa idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu imeendelea kuongezeka na kufika 78,429 mwaka 2024. Alisema serikali imetenga jumla ya shule 6088 zinazopokea wanafunzi hao na kuwapatia Afua stahiki na miongoni mwa shule hizo, shule 309 zina mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.

Kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini, serikali imejenga shule mbili maalumu za mfano moja wapo ni shule maalumu ya Patandi.

Alisema serikali imedhamiria kuwapatia taaluma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kuhakikisha wanapata chakula cha uhakika kwa kutoa ruzuku kwa mwanafunzi wa kutwa na bweni 

Awali Mkurugenzi wa elimu maalumu, dkt. Magreth Matonya kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia, alisema maadhimisho hayo ya miaka 30 katika shule maalumu ya patandi yametokana na kuanza utekelezaji wa elimu jumuishi nchini ambapo Tanzania ilisaini mkataba wa kimataifa mwaka 1994.

"Maadhimisho haya yana malengo manne, kutangaza fursa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kutangaza mafanikio, kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wazazi wanaowaficha watoto na kutoa tathimini tulipo na tunapoelekea"

Dkt Matonya alisema dhana ya elimu Jumuishi ni kuwaweka pamoja wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wasio na mahitaji maalumu waweze kusoma kwa kutegemeana na kusaidiana

Alisema tangia kuanza kwa mpango huo wa elimu jumuishi serikali imefanikiwa maeneo 36 ikiwemo kuanzisha kamusi ,kuboresha vyuo vya ualimu ambapo mwaka 2024 jumla ya walimu 768 wamehitimu pia ununuzi wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji.

Alisema  nchi yetu Tanzania elimu Jumuishi ilianza kutekelezwa muda mrefu kupitia sera ya elimu ya mwaka 1978 iliyoelekeza upatikanaji wa elimu kwa kila mtoto,utekelezaji wa sheria hiyo kwa watoto wenye mahitaji maalumu umerasimishwa mwaka 1998 kupitia mradi wa wizara ya elimu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la elimu , sayansi na utamaduni (UNESCO).

"Katika Taifa Letu bado tuna watu wenye kufikiri kwamba mtoto mwenye changamoto hana haki ya kupata elimu, nichukue nafasi hii kuwaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, wekeni utaratibu wa kufuatilia jamii hiyo kuanzia ngazi ya makazi ya wananchi kama kuna mtoto mwenye changamoto amefichwa serikali ichukue hatua mara moja"

Waziri amesema kuwa idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu imeendelea kuongezeka na kufika 78,429 mwaka 2024.Alisema serikali imetenga jumla ya shule 6088 zinazopokea wanafunzi hao na kuwapatia Afua stahiki na miongoni mwa shule hizo, shule 309 zina mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.

Kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini, serikali imejenga shule mbili maalumu za mfano moja wapo ni shule maalumu ya Patandi.

Alisema serikali imedhamiria kuwapatia taaluma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kuhakikisha wanapata chakula cha uhakika kwa kutoa ruzuku kwa mwanafunzi wa kutwa na bweni.

Awali Mkurugenzi wa elimu maalumu, dkt. Magreth Matonya kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia ,alisema maadhimisho hayo ya miaka 30 katika shule maalumu ya patandi yametokana na  kuanza utekelezaji wa elimu jumuishi nchini ambapo Tanzania ilisaini mkataba wa kimataifa mwaka 1994.

"Maadhimisho haya yana malengo manne, kutangaza fursa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kutangaza mafanikio ,kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wazazi wanaowaficha watoto na kutoa tathimini tulipo na tunapoelekea"

No comments: