DC SHAKA - TUNAUNDA KAMATI MAALUM KUCHUNGUZA KIFO CHA MJAMZITO WANANCHI KUWENI NA AMANI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 11 September 2024

DC SHAKA - TUNAUNDA KAMATI MAALUM KUCHUNGUZA KIFO CHA MJAMZITO WANANCHI KUWENI NA AMANI

 




Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amelazimikia kuunda kamati maalum  ya kuchunguza chanzo cha kifo cha mama mjamzito kinachodaiwa kutokea kwa kucheleweshewa huduma baada ya kukosa fedha ya mafuta ya gari la wagonjwa(Ambulance) kiasi cha shilingi laki moja na themanini.


Mjamzito huyo inadaiwa alisema rufaa kutoka kituo cha afya Kidodi kwenda hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo mji mdogo wa Mikumi.


Aidha maamuzi  ya mkuu wa Wilaya huyo Shaka aliyatoa Jana kwenye mkutano wa hadhara, na  yamekuja baada ya mwanaume mmoja aliyefahamika Kwa jina Seleman Makuani kulalamika kuwa mkewe alicheleweshwa kupatiwa usafiri wa gari la wagonjwa kwa kukosa fedha hiyo katika kituo cha Afya Kidodi baada ya kupewa Rufaa hadi alipotoa shilingi laki moja ndipo alipopatiwa usafiri huo.


Alisema baadae mkewe alifariki baada ya kufikishwa katika hospital ya Mtakatifu Kizito Mikumi ikiwa ni zaidi ya saa tano tangu afikishwe katika kituo hicho cha Afya.


Kufuatia hatua hiyo Shaka alilazimika kusitisha mkutano wa hadhara alikokuwa akisikiliza kero za wananchi na kulazimika kuitisha kikao cha kamati ya Usalama wa Wilaya cha dharura ili kutafakari kadhia hiyo na kuja na majibu ambayo wananchi wote walipokea na waliridhia kwa shangwe kww uamuzi huo. 


Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kidodi Elia Mwakibete alusema gari hilo la wagonjwa halikuwa na mafuta hata dereva Bado hajaletwa hivyo wanalazimika kukosa madereva wa nje ya Serikali .


Baaada ya malalamiko hayo DC Shaka akaunda kamati maalum ya inayohusisha pia vyombo vya ulinzi na Usalama kuchunguza jambo hilo ambapo kamati ilianza kazi siku hiyo hiyo na inatakiwa kukabidhi ripoti yake kwa mkuu wa Wilaya baada siku tatu ili kubaini ukweli na uhalisia na tukio hilo. 


Mwisho..

No comments: