Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
RAIA 12 wa Burundi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma ya kuingia nchini bila kibali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama alisema hayo jana mjini hapa wakati akitoa taarifa ya mafanikio katika oparesheni zinazoendelea ambazo zinalenga kutanzua na kuzuia uhalifu mkoani hapo.
Kamanda huyo aliwataja waliokamatwa ni Tusenge Juvenal(25),Nshimumukiza Eloje (20), Nibizi Elia (30),Nduwayo Ally (21), Niyomwungere Jabal (18), Nimbona Pierre (34), Ndayishimye Jean (20), Kamaliza Geraridine (28), Niyonizeye Sandrine (8), Kezakimana Lidia (6), Miburo Malitha (4),na Josefu Nikora (14)
Aidha alisema watuhumiwa wote wamekamatwa Septemba 4, 2024 huko kata ya Dakawa Wilaya ya Mvomero wakiwa wanafanya kazi katika mashamba ya miwa .
"Mafanikio hayo ni pamoja na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo, usimamizi wa kesi mahakamani na oparesheni za usalama barabarani. "alisema.
"Oparesheni hii imefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili wengine wawili wanaojihusisha na matukio ya ujambazi katika maduka"alisema.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni waliokamatwa ni Joseph Kusekwa (55) mkazi wa Mgudeni ambaye alikamatwa akiwa na mali za duka zilizoibiwa katika duka la Leonard Mhina (40) mfanyabiashara mkazi wa Mnyunywe kata ya Maguha Wilaya Kilosa.
Alisema katika Wilaya ya Kilombero
alikamatwa Jofrey Sixbert (21) mkazi wa Kiberege aliyekuwa anatafutwa kwa matukio ya ujambazi akiwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni Simu, TV, Sabufa na funguo 70 zinazofungua milango mbalimbali.
Aidha alisema mafanikio yamepatikana katika doria na misako dhidi ya wezi wa mifugo ambapo Septemba 7, 2024 katika kijiji cha Msolwa kata ya Ruhembe Jeshi la Polisi lilifanikiwa walikamatwa watuhumiwa watatu ambao ni wezi wa mifugo.
Watuhumiwa wengine walikamatwa Septemba 3, 2024 wakiwa na nyama ya ng’ombe zilizochinjwa baada ya kuiba ng’ombe 14 mali ya Lucas Kazimoto .
Aliwataja watuhumiwa walikutwa wakiuza nyama ya ngo’ombe, ikiwa ni sehemu ya ile iliyoibwa
Waliokamatwa ni Yohana Sambuka Mliga (22) mkulima mkazi wa Zombo Christian Damian Mgomi (41) mkazi wa Madizini, Mohamed Kibwana Mnazi (40) mkulima mkazi wa Madizini, Christian Damian Mgomi (41) mkazi wa Madizini wilayani Mvomero .
Wakati huo huo kamanda huyo alisema . madereva wanne (4) wamefungiwa leseni zao na kati ya hao wawili (2) wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya usalama barabarani ikiwemo mwendokasi.
Alisema oparesheni ya usalama barabarani imehusisha ukamataji wa pikipiki 52 na bajaji 22 zinazojihusisha na uhalifu. Miongoni mwa pikipiki hizo ni zile zinazokatwa bomba la moshi ambazo husababisha kelele zinapopita barabarani.
Aidha, waendeshaji wasio na leseni wametakiwa kujiunga na mafunzo ya udereva kabla ya kuadhibiwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment