KIJANA COSTA AKUTWA AMEFARIKI ENEO LA MASEYU PEMBENI YAKE KUKIWA NA PIKIPIKI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 16 September 2024

KIJANA COSTA AKUTWA AMEFARIKI ENEO LA MASEYU PEMBENI YAKE KUKIWA NA PIKIPIKI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


KIJANA aliyefahamika kwa jina la Costa  Clemence (22) mkazi Maseyu kata ya Gwata wilaya ya Morogoro amafariki dunia  na mwili kukutwa umetelekezwa eneo la Maseyu kijiji cha Gwata.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mkoani hapa na Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama ilisema mwili wa kijana huyo ulikutwa amefariki dunia Septemba 15 mwaka  huu majira asubuhi huko Gwata huku pembeni yake kukiwa na pikipiki isiokuwa na namba za usajiri ambayo inasadikiwa kuwa ni ya marehemu mwenyewe.


Mkama alisema mwili huo ulikutwa eneo hilo la Gwata ambalo halina makazi ya watu na kwamba mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.


"Niwaombe tupeni muda tunalifanyia kazi, uchunguzi ukikamilika tutawapa taarifa kamili hakuna kitu kitakachofichwa," alisema kamanda Mkama,


Naye  mwenyekiti wa kijiji cha Gwata Ally Gobole alisema usiku wa kuamkia Septemba 15 mwaka huu walifika watu wasiojulikana  nyumbani kwao Marehemu na kumchukua kisha kutokomea kusikojulikana.


Gobole alisema baba wa marehemu alitoka nje  na kuona watu hao wakitokomea na kijana wake akaanza kuwakimbiza bila mafanikio na hivyo kutoa taarifa kwa mwenyekiti  wa kijiji.


Alisema katika tukio hilo walichukuliwa vijana wengine  watatu akiwemo Azizi Kimweru akiwa barabarani ananunua chips kisha wakamchukua mwingine aitwaye Malinda maarufu kama Jack wakaondoka nao na kwenda kuwapiga .


Alisema vijana hao wawili ambao ni Jack na Azizi wapofutiliwa walikutwa wamepigwa na kuumizwa vibaya ambao walitoa taarifa ya kifo cha mwenzao huyo Costa na ndipo mwenyekiti na wananchi walitoka kuanza kumtafuta na hatimaye kumkuta amefariki.


Mwenyekiti huyo alisema majeruhi hao wamelezwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.


MAIPAC Itaendelea kuwajuza wasomaji wetu juu ya tukio hilo.


Mwisho.

No comments: