PAuline Gekul Aja Na Mama Samia Cup Kuvumbua Vipaji vya Soka Mjini Babati - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 20 September 2024

PAuline Gekul Aja Na Mama Samia Cup Kuvumbua Vipaji vya Soka Mjini Babati

 





Na Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Zaidi ya Jezi 86 pamoja na mipira zimetolewa kwenye kata mbalimbali Mkoani Manyara kwaajili ya kuibua vipaji kwa Vijana katika michuano ya mpira wa miguu kwa lengo la kupata timu bora na imara ambayo itacheza ligi kuu soka Tanzania.


Michuano hiyo ya ngazi ya Jimbo la Babati Mji, imepewa jina la Mama Samia na gekul cup imezingatia makundi yote ikiwemo,boda boda, taasisi mbalimbali pamoja na Vijana Chini ya umri wa miaka 15. 


Akizungumza wakati wa ugawaji wa Jezi hizo, Mbunge wa Babati Mji Pauline Gekul amesema lengo la michuano hiyo ni kuibua vipaji kwa Vijana ndani ya Mkoa kwa manufaa ya Taifa na kwamba Vijana hao pia waweze kutumia uwanja wao wa Tanzanite kwaraa uliojengwa.


"Hata hivyo tunatimu zetu ambazo tayari zipo katika Mji wetu wa babati,tuna babaji,aah veta,Tutawapatia Jezi zao za heshima zao,kila timu ya Kijiji na Kila timu ya Mtaa iweze kuwaibua Vijana wadogo  wa miaka 15,ili tuweze kuwa na timu za makundi yote Yani timu za taaasi hizi,na timu zilizotoka kwenye kata".


Amesema ni fursa kwa wazazi wenye watoto wenye kipaji Cha mpira  kujitokeza kwa wingi na kujiunga kwenye mashindano hayo kwakua ni manufaa kwa Kila mmoja na Taifa kwa ujumla.


"Kupitia kijiji na Kila Mtaa tutawapa Jezi na mpira watachuana huko,watacombine huko na watatuletea timu ya kata,na itakwenda kushindana na kata nyingine baada ya hapo tutapata heros nao tutawalea na kuwamotive ili tupate sasa timu ya jimbo".


Mbunge Gekul ametumia fursa hiyo na kusema kwamba wakati wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa michuano hiyo itatumika kama chachu ya kuhamasisha Uchaguzi.


Aidha,Mwenyekiti Chama Cha mpira wa miguu Wilayani Babati Mkoani Manyara Gerald Mtui amesema vilabu vingi vimepokea kushindana kwa mashindano hayo na kwamba mgawanyiko wa viwanja kwa Kila Mtaa na Kila kata umejipanga vizuri.


November 2,2024 ni fainali za Jimbo kwa michuano hiyo huku ikielezwa zawadi kwa timu itakayoshinda inaendelea kuboreshwa na kwamba ushindi wa timu hiyo itajofungulia fursha katika kushiriki michuano ya Kitaifa.

No comments: