Naibu Waziri Sillo Awaonya Madereva Wazembe Wanaosababisha Ajali - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 1 September 2024

Naibu Waziri Sillo Awaonya Madereva Wazembe Wanaosababisha Ajali

 




Na Epifania Magingo,Babati.


maipacarusha20@gmail.com 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Daniel Sillo amesema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua  madereva wazembe wasiotii Sheria za usalama barabarani.


Ameyasema hayo  alipowatembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Wilayani Babati ambapo amebainisha kuwa hali zao zinaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu ya awali.


"Kuzingatia sheria za barabarani ni pamoja na kuzingatia kuendesha gari kwa umakini, kufuata alama za barabarani na kuendesha kwa tahadhali ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika"Alisema Sillo.


Kwa mujibu wake madereva wasio na leseni hawaruhusiwa kuendesha vyombo vya moto kwa kuwa ni chanzo cha ajali za barabarani.


Majeruhi wa ajali hiyo ya gari iliyotokea  Agosti 31,2024 Kijiji cha Gajal wilaya ya Babati ilitokea,baada ya gari aina ya Costa yenye namba za usajili T 187 DXV kugongana na gari la mizigo Scania lenye tela namba za usajili RL 5485.


Waliofariki katika ajali hiyo ni wanafunzi watatu wa kike  ambao walijulikana kuwa ni Lyidia Saitoti, Aisha Rahimu, Samira Khalid na dereva wa gari hilo,Abdul Abdallah.


Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara kamishna msaidizi mwandamizi Ahmed Makarani alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari hilo aina ya Scania aliyehama upande wake bila kuchukua tahadhari.


"Kati ya wanafunzi 30 waliojeruhiwa 5 wameumia vibaya na kulazwa katika wodi ya dharura (ICU) katika hospitali hiyo ambapo "Wanafunzi 33 waliokuwa katika ajari ni wanafunzi 3 pekee ni wanaume na kati ya hao waliokufa ni wanafunzi wakike watatu" Alifafanua Makarani.


Kamanda aliwataka madereva na watumia barabara kuwa  waangalifu pindi wanapoendesha ili kuepuka ajali zinazosaabisha vifo vya watu na ulemavu wa kudumu.


Hata hivyo Kamanda alisema dereva huyo wa lori raia wa Burundi baada ya kusababisha ajali alikimbia na jitihada za kumtafuta zinaendelea.


Naye diwani wa kata ya Dareda, Sabini John alisema eneo hilo la Gajal lenye mlima na mteremko mkali lina historia ya ajali za mara kwa Mara.

No comments: