NAMUNGO WAAPA KUIFUNGA DODOMA JIJI UWANJA WA QUARAA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 11 September 2024

NAMUNGO WAAPA KUIFUNGA DODOMA JIJI UWANJA WA QUARAA

 



Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com

Timu ya Namungo Fc imetamba kuifunga Timu ya Dodoma Fc Katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara (NBC)mchezo utakaopigwa dhidi ya mechi hizo mbili kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara September 12 ,2024.


Klabu hizo zinakutana uwanjani zikiwa na rekodi ya kutofanya vizuri kwa mechi mbili zilizopita kwa Kila timu huku ikielezwa kuwa kwa mchezo unaofuata  Dodoma Jiji watakuwa wenyeji wa mchezo dhidi ya Namungo.


Makocha wa timu hizo mbili wamezunguza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kocha wa Namungo Mwinyi Zahera amesema kikosi kimejipanga vizuri katika kuchua alama tatu muhimu kwakua wachezaji wamefanya mazoezi ya kutosha na kua na nidhamu nzuri mchezoni.


"Ugumu wa mechi nadhani kama utakua fifty fifty na wachezaji tunao na hatuna shida yoyote na maandalizi jinsi tulijiandaa nadhani tulikua tofauti kidogo na ile mechi ya kwanza lakini kwa hii ya kesho nadhani tutakuwa vizuri".


Aidha,Kocha Mzawa wa Timu ya Dodoma Jiji Fc Mecky Maxime amesema timu hiyo imekuja kuleta burudani  na kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo.


"Kikubwa tumekuja kuwaletea burudani Dodoma Jiji ni timu yenu ,njoeni muishangilie najua nyinyi mkija pale mnakuwa kama mshabiki wa kumi na mbili tulichokiandaa mje mkione".


Kwa upande wa Nahodha wa Timu ya Namungo Fc Erasto Edward Nyoni amesema  wachezaji wamejiandaa vizuri kwenye mchezo huo na kutarajia mechi itakua nzuri na kupata matokeo mazuri,huku Nahodha wa timu ya Dodoma Jiji Fc Augustino Msata  amesema wanaamini kupata matokeo mazuri kwakua wanaenda kukutana na mpinzani aliefanya vibaya kwenye mchezo uliopita.

No comments: