RAIS SAMIA ATOA POLE KWA WAKULIMA LUHEMBE KILOSA KUUNGULIWA MIWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 25 September 2024

RAIS SAMIA ATOA POLE KWA WAKULIMA LUHEMBE KILOSA KUUNGULIWA MIWA

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


RAIA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa wakulima wa Miwa wa kijiji Cha Luhembe Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro baada ya mashamba yao kuteketea kwa moto.


Hekari za mashamba ya Miwa zaidi ya 1,000 ziliunguabkwa moto ambazo ni sawa na tani Elfu thelathini(30) yenye thamaninya sh bilioni 3.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Dennis Londo alifikisha salamu za Rais kwa wakulima hao Jana baada ya kufika kijijini hapo.


Londo alisema"Rais anawapa pole sana wakulima na ametaka mwekezaji kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha Miwa ya wakulima inakatwa ili kuondoa hasara ya wakulima na kuondolewa shambani na kuipeleka kiwandani kwa haraka,".


Alisema mwekezaji tayari ameanza kutekeleza maagizo ya Rais na  taratibu ya kuondoka Miwa ya wakulima shambani na kuipeleka kiwandani.


Amemshukuru Rais, na mwekezaji kwa kutekeleza maelekezo ya Rais na kuyafanyia kazi kwa haraka

kwa kusimamisha shughuli zote za ukataji wa Miwa kawaida na kuelekeza nguvu kwenye kukata Miwa iliyoungua pekee na kupelekwa kiwandani.

....

No comments: