BITEKO AZINDUA MASHINDANO YA SHIMIWI,ATAKA MAELEZO KWA VIONGOZI WA TAASISI WALIOSHINDWA KUSHIRIKI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 25 September 2024

BITEKO AZINDUA MASHINDANO YA SHIMIWI,ATAKA MAELEZO KWA VIONGOZI WA TAASISI WALIOSHINDWA KUSHIRIKI

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


NAIBU Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dk Dotto Biteko ameonyesha kukasirishwa na baadhi ya wakuu wa taasisi walioshindwa kutoa vibali na Fedha kwa watumishi wao kushiriki michezo ya  SHIMIWI.


Aidha Naibu Waziri mkuu Dk Biteko amemwagiza katibu mkuu utumishi kumpa taarifa za kutosha kwa wote walioshindwa kuhudhulia Michezo hiyo.


Dk Biteko amesema hayo mjini Morogoro wakati akifungua Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) iliyoshirikisha vilabu 57 inayojumuisha mikoa 16, wizara 24,na idara zinazojitegemea 6 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri


Aliwaagiza makatibu wa Wizara kuwaruhusu watumishi kushiriki kwenye mashindano hayo kutokana ushiriki kupungua mwaka huu.


Alisema kuwa mwaka jana vilabu vilivyoshiriki vilikuwa 74 lakini kwa mwaka huu ni vilabu 57 pekee vilivyoshiriki mashindano hayo ambayo wakala wa serikali 3 na taasisi za umma 8.


Naibu Waziri Mkuu,Dk.Buteko alifungua mashindano hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassa n na kuwataka makatibu wa Wizara kubadilika kwa kuwaruhusu watumishi kushiriki kwenye michezo ya shirikisho kutokana na ushiriki watumishi kushuka ikiringanishwa kwa mwaka jana.


Mashindano hayo yalishirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,pete,kuvuta kamba, baiskeri na michezo ya jadi,kwamba licha ya mwaka jana  kuwahimiza lakini mwitikio wa mwaka huu yamepungua.


Awali, mwenyekiti wa Shimiwi,Daniel Mwalusamba alishukuru ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na benki ya NMB ambayo imekuwa kudhamini mashindano hayo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.


Mwalusamba alitaja wadhamini wengine ni Osha,ambalo kila mwaka walikuwa wakidhamini bonanza yanayoratibiwa na shirikisho hilo,ambapo aliwaonesha wakazi wa Mkoa wa Morogoro kujitokeza katika kuunga mkono mashindano hayo kwa kufikia uwanjani kushuhudia.


Kwa upande wake Naibu waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan kumekuwa na matokeo mazuri katika maendeleo ya Klabu kwa kufanya vizuri,hususan timu ya Yanga na Simba.


Mwinjuma alisema kuwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa kulikuwa na ‘Ubaya Ubwela’ mwingi kutokana na Simba kufanya vizuri na Timu ya Yanga kutokana na ubora waliounesha na kufuzu kuingia kwenye makundi.


Alisema kuwa timu ya taifa ya mpira wa miguu  ilitoka hivi karibuni kushiriki mashindano ya Afrika kwenye Ivory coast kwamba kutokana na hamasa ya michezo inayofanywa na Rais Samia ni wazi kuwa kuna viashiria kuwa taifa stars ifanya vizuri katika mashindano hayo nchini Morocco Mwakani.


Mwisho.

No comments: