![]() |
| Mbunge wa Monduli Fred Lowassa akikabidhi vitimwendo kwa watoto wenye ulemavu Kijiji Cha Mbuyuni kata ya Makuyuni wilayani Monduli |
![]() |
| Mbunge wa Monduli Fred Lowassa akimpongeza Mkurugenzi wa SYWSO, Omega Mlay kwa kutimiza matendo ya huruma kwa watoto wenye ulemavu katika Kijiji hucho |
Mwandishi Wetu, Monduli
maipacarusha20@gmail.com
Mbunge wa Monduli Fred Lowassa amewataka Watanzania kumuenzi Dr. Reginald Mengi kwa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwepo wenye ulemavu ili wajikwamue kwenye umasikini.
Lowassa ametoa maombi hayo kwenye uzinduzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Smile Youth and Women Support Organization (SYWSO) katika Kijiji Cha Mbuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
Amesema Shirika la (SYWSO) limefanya tendo la huruma kwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kwa kuwapatia viti mwendo, fimbo za walemavu na vifaa vya shule kwa watoto hao wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa Shirika la SYWSO, Omega Mlay amemwambia mbunge huyo kuwa baada ya kushirikiana na Serikali ya Kijiji hicho walipata idadi ya watoto wenye ulemavu na kuomba sapoti Matt Foundation waliomsaidia Kutoa vitimwendo kwa watoto hao na kuwawezesha kwenda shule.
Mkurugenzi huyo alimuomba Mbunge huyo Kutoa sapoti ya bima ya Afya kwa watoto ishirini wenye ulemavu waliopo katika Kijiji hicho ili waweze kupata huduma ya Afya kwa uhakika.
Mbunge huyo alitimiza ombi Hilo kwa Kutoa kiasi Cha Shilingi milioni Moja kwa ajili ya bima za Afya kwa watoto hao wenye ulemavu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd yenye makazi yake Babati Mkoani Manyara David Mulokozi, Bwana Izaki Piganio Afisa miradi Matt foundation alisema kampuni hiyo kutokana na faida wanayopata wameamua kutenga fedha kusaidia jamii.
Alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa jamii na baada ya kupokea maombi ya SYWSO waliamua kukubali na kuwasaidia watoto na watu wenye ulemavu katika Kijiji hicho.
Katika uzinduzi huo Taasisi ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) ilizindua pia mpango wa kugawa majiko ya gesi bure kwa jamii za pembezoni ili kuanza kutumia nishati safi na salama.
MAIPAC walitoa majiko ya gesi kuwawezesha wakina Mama wa Jamii hiyo kuepuka matumizi ya Kuni ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Mussa Juma Mkurugenzi wa Maipac amesema kuwa wao kama washirika wa SYWSO wanaunga mkono kwa kutoa majiko hayo ili kuendana na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wengi wanatumia Nishati safi ya Kupikia.
Juma alisema katika mpango huo wanakusudia kugawa bure majiko zaidi ya 1000 kwa jamii hizo ambazo zinapakana na Hifadhi za Taifa, Mapori ya akiba na hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA).
Mwisho

| Mbunge Fred Lowassa, Mkurugenzi wa SYWSO Omega mlayi na afisa masoko wa matt foundation wakimkabidhi Mmoja wa akina Mama jiko la gesi |
![]() |
| Mbunge Fred Lowassa pamoja Mussa Juma Mkurugenzi wa Maipac wakimkabidhi Mmoja wa wamama jiko la gesi |
Katika uzinduzi huo Taasisi ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) ilizindua pia mpango wa kugawa majiko ya gesi bure kwa jamii za pembezoni ili kuanza kutumia nishati safi na salama.
MAIPAC walitoa majiko ya gesi kuwawezesha wakina Mama wa Jamii hiyo kuepuka matumizi ya Kuni ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Mussa Juma Mkurugenzi wa Maipac amesema kuwa wao kama washirika wa SYWSO wanaunga mkono kwa kutoa majiko hayo ili kuendana na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wengi wanatumia Nishati safi ya Kupikia.
Juma alisema katika mpango huo wanakusudia kugawa bure majiko zaidi ya 1000 kwa jamii hizo ambazo zinapakana na Hifadhi za Taifa, Mapori ya akiba na hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA).
Mwisho

No comments:
Post a Comment