![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda |
Na Queen Lema, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wanasiasa wote wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kupeleka maendeleo mbele kwa wananachi wote bila kubagua na hata kama wanapingana kwa hoja mbalimbali kwani Kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi utasababisha kuendelea kukithiri kwa umaskini
Endapo kama kutakuwa na ubaguzi wa kisiasa miradi mbalimbali ambayo imelengwa kutekelezwa na serikali haitaweza kutekelezwa ipasavyo
Makonda amesema hayo jana kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba miwili ya soko la machinga ,pamoja ujenzi wa uwanja wa mpira Ambao unatarajia kuanza
Makonda alisema kuwa ni vibaya Sana Kwa wanasiasa kuacha kutekelezwa miradi kwaajili ya matakwa Yao Jambo ambalo linachangia sana kuchelewesha maendeo ya wananchi
"Siasa lazima iwepo lakini tofauti za kisiasa zisitufanye tuache kuchochea maendeleo mfano kuna huu mradi.wa soko serikali ilishatoa ela yote toka 2021 lakini haukufanikiwa na hili limefanikiwa leo kuweza kutokea kwa sababu nimesimama ipasavyo naomba sana hili lisijitokeze tena serikali inapoleta fedha inalenga wote aichagua kuwa wewe upo kambi ipi na ipi"aliongeza Makonda
Aliendelea kwa kusema kuwa Kwa mkoa wa Arusha kwa sasa Agenda kubwa ni maendeleo kwa kuwa Arusha ni miongoni mwa Mikoa ambayo inavutia sana kwenye sekta ya uchumi lakini hata utalii.
"Natamani sana kuona kila MTU ananufaika na wageni ambao wanaokuja Arusha na watanufaika tu endapo kama kutakuwa na uwiano mzuri Kati ya mtendaji wa Serikali lakini pia mwanachi nataka kila MTU asimame kwenye sehemu yake"aliongeza Makonda.
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuatilia miradi mbalimbali ambayo imesainiwa na endapo kama mkandarasi ataonesha kusuasua basi watoe taarifa mara moja.
"Arusha kulikuwa na tabia ya kusaini mikataba kwa kificho kikubwa lakini Mimi nimekuja na hii Mimi Mambo yote hadharani ili wananchi waweze kujua na kutambua kuwa kulikuwa na mradi na wao sasa wataweza kuyafutilia kwa ukaribu sana "aliongeza
Naye mmoja wa wazubuni waliweza kushinda kwenye zabuni ya ujenzi wa soko la machinga ambao ni kampuni ya Suma Jkt construction Ltd walisema kuwa watahakikisha wamemaliza mradi huo ndani ya muda muafaka
Luteni Kanali Daudi Zengo alisema kuwa pamoja na kuwa wameshinda zabuni hiyo watafanya kwa uimara mkubwa sana kwa kuwa wao wanatekeleza shuguli mbalimbali za miradi
Luteni Kanali Zengo alisema kuwa Jiji la Arusha wamewaamini kwenye katika mradi huo na wao watahakikisha kuwa wanakuwa wanatekeleza mradi huo vyema
"Suma Jkt ni kampuni ya kizalendo na itafanya kazi kwa uzalendo mkubwa sana na kwa mradi huu tunatarajia kumaliza hata kabla ya wakati ili wananchi waweze kunufaika"aliongeza
Mwisho

No comments:
Post a Comment