MISA-TAN, EWURA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUWASILISHA MALALAMIKO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 16 June 2025

MISA-TAN, EWURA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUWASILISHA MALALAMIKO


Mwenyekiti wa MISA- Tan Edwin Soko

Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki

 
Wanacahama wa MISA-Tan wakisikiza mada



NA: Andrea Ngobole, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Watumiaji wa Huduma za nishati na maji nchini wametakiwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA ambayo yemeshindwa kutatuliwa na watoa huduma za nishati na maji ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza katika semina elekezi kwa wanachama wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki Nyarabu Musira amesema bado jamii kubwa ya watanzania hawajaelewa majukumu ya EWURA hivyo kuwataka waandishi wa habari kwenda kuwaelimisha wananchi kuifahama EWURA na majukumu yake.


 "Jukumu letu EWURA ni Kutoa elimu kwa umma juu ya  na kupitia nyinyi waandishi na wanachama wa MISA- Tan tunaamimi umma utaenda kufahamu vema majukumu ya EWURA kwa yoyote mwenye Malalamiko dhidi ya huduma za nishati na Maji" alisema 

Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania MISA- TAN Edwini Soko amesema lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uwezo na kuchechemua misingi ya kazi za waandishi wa habari kwenye kuleta maendeleo .
 
"Ndugu wanachama mafunzo haya ni muhimu sana kwetu wanahabari ili tuandike habari sahihi kuhusu Ewura na majukumu yake, ni Matumaini yangu Kila moja HAPA atakuwa mwakini kwenye kuandika  na kuelezea kwa kina majukumu ya Ewura kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla" Alisema Mwenyekiti huyo

 Baadhi ya wandishi habari waliopatiwa semina hiyo wameelezea namna watakavyoenda kutumia kalama zao kuelimisha jamii juu ya shughuli zinazofanywa na EWURA na namna bora ya kutoa malalamiko yao pindi wanapopapata changamoto huduma wanazozitumia

Mwavita Mkondo  amesema kuwa mafunzo hayo yamempa.mwanga mkubwa wa namalna Ewura inavyofanya kazi na kwa Sasa atakuwa makini kwenye kuelimisha umma pale unapopata changamoto katika sekta ya maji na au nishati.

Mapuli Misalaba Mwandishi  wa Misalaba media amesema kuwa ni mafunzo  muhimu kwake na kwa Sasa amepata uelewa mpana wa namna ya kuandika habari za Ewura.



No comments: