
Burhani Yakub,Tanga.
maipacarusha@gmail.com
Mwanachama wa Chama Cha Demokrasiaa na Maendeleo (Chadema) na mwanaharakati.Lulu Mapunda (Aunt Lulu) amewataka walioamua kufanya maandamano keshokutwa Jumatano wapishe kwanza uchaguzi ndipo watimize azma hiyo.
Amesema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Tanga.
Amesema yeye alikuwa kinara na mhamasishaji maarufu wa maandamano lakini ametafakari kwa kina na kubaini kuwa maandamano yataleta madhara makubwa kuliko faida.
Badala yake amewataka watanzania kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura Ili wawachague wagombea wanaoona watawaongoza.
Amezitaja athari zitakazojitokeza iwapo watu wataandana kama alivyokuwa akihamasisha awali ni kuwa licha ya kumwaga damu kwa waandamanaji pia utatokea uporaji wa mali za wananchi.
"Nimetafakari na kuona ni vyema tusubiri uchaguzi huu ufanyike ndipo tuitishe maandamano...hapo tutakuwa tumeepusha mambo mengi yakiwamo ya umwagaji damu kwa ndugu zetu ambao hawana uwezo wa kukimbilia nje ya nchi"amesema Anti Lulu.
Mwanaharakati huyo amewataka wenzake ambao wamekuwa wakoshirikiana kuhamasisha maandamano kuacha Kwa sababu baadhi wako nje ya nchi ambako hawawezi kupata madhara.
"Wenzetu wako nje ya nchi kama wana nia njema waje tuungane katika maandamano haiwezekani wao wako mbali watuhamasishe sisi tutoke kuandamana"amesema Lulu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment