MGOMBEA URAIS CUF AWATAKA WANANCHI KUTONUNULIWA NA KUPEWA RUSHWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 23 October 2025

MGOMBEA URAIS CUF AWATAKA WANANCHI KUTONUNULIWA NA KUPEWA RUSHWA

 


Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


MGOMBEA urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo amewataka wananchi kuacha kununuliwa kwa kupewa rushwa na baadae kulalamika kwa matatizo yanayowapata kama kukosa maji,huduma za Afya,Ajira na miundombinu Bora.


Amesema hayo mkoani Morogoro wakati akifanya mkutano na Waandishi wa habari ambapo anayarajiwa kufanya mikutano ya hadhala katika Kata za Mzinga, Kauzeni na standing ya zamani ya Manispaa ya Morogoro.


Gombo alisema watanzania wamekuwa wakilalamikia sana kwa kutooata huduma za msingi, lakini Cha kudhangaza wamekuwa hawatimizi wajibu wao.


"Leo ni siku ambayo mawakala wanaapa na mpaka Sasa watakuwa wameapa,nimepata taarifa baadhi ya majimbo ambao sisi tumesimamisha wagombea mawakala wetu wamenunuliwa na hawajajitokeza wamekataa kwenda kuapa, wanaendekeza sana vitushwa," alisema.


Mgombea huyo Urais alisema watanzania wamekuwa wakilalamikia hawana barabara nzuri lakini unapofika uchaguzi badala ya kwenda kupiga kura na hawashawashiki wao ndo kwanza wanapokea rushwa.


Alitolea mfano wa Moja ya jimbo ambalo walisimamisha wagombea 15 kuwa Sasa wamebaki 5 tu na walikuwa wamewaweka mawakala zaidi ya 500, mawakala zaidi ya 300 wamenunuliwa na kugoma kwenda kuapa


"Kama tabia ya kupokea rushwa haitaisha na kama wanataka mabadiliko ya kweli waachane na tamaa ndogondogo na kuuza utu wao,baadhi ya vyama kwa Sasa vinaangalia maslahi yao,"alisema


Alizungumzia suala la wananchi kujitokeza kupiga kura na kutoogopa vitisho vya baadhi ya watu vinavyoendelea hasa kwenye mitandao, na kwamba hakuna njia mbadala kwao.


Aliwaomba watanzania kuwa hakuna namna yoyote ya kuweza kupata viongozi wao na kuacha kusikiliza kitu chochote,na badala yake waende wakapige kura kwa kutaka haki ambayo italeta Amani.


Pia mgombea huyo wa Urais alisema baada ya yeye kupata ridhaa ya kuwa Rais atahakikisha anafanya mabadiliko ya katiba na kuweka mambo ya msingi kwa faida ya nchi.


"Nitabadikisha katiba ya Tanzania ili nitoe mwongozo mzuri na kutengeneza mifumo wa kutenda haki, kwamba kwa sasa katiba haina ukomo wa kutawala nchi kwa chama lazima ifike mahali vyama view vinafika ukomo,"alisema.


Gombo akazitaka TAKUKURU na INEC kutenda haki kwa kuzingatia  wajibu wao bila kuangalia chama gani kinatenda makosa bila kuwepo kwa upendeleo wowote.


"Katika katiba kuna mambo mengine nitarekebisha kama sio kuifuta TAKUKURU kwa sababu kimekuwa chombo hakionekanani kinafanya kazi gani kinachoshughulikia vitushwa vidogo,"alisema.


Oktoba 29,2025 Tanzania itakuwa na uchaguzi mkuu ambapo watanzania wametakiwa kujitokeza kupiga kura.


Mwisho.

No comments: