Na Queen Lema na Andrea Ngobole,Monduli
maipacarusha@gmail.com
RAISI wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Dkt Samia Suluhu Hasani Amewatunuku kamisheni maafisa wapya 296 wa kundi la 06/22 shahada ya sayansi ya kijeshi (BMS). na kundi la 72/24 Regular katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha
Aidha maafisa hao wapya wamekuwa maafisa wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika cheo cha luteni USu huku kundi la 06/22-BMS wakiwa wamepata mafunzo kwenye chuo hicho kwa muda wa miaka mitatu.
Kabla ya kutunuku kamisheni mheshimiwa Raisi na Amiri Jeshi mkuu alikagua gwaride maalumu lilioandaliwa na maafisa wanafunzi kutokana na maelekezo maalumu ya mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli, Meja Jenarali Jackson Mwaseba.
mbali na hayo pia Raisi Samia pia aliweza kutoa zawadi kwa maafisa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi huku kwenye kundi la 06/22;BMS aliyefanikiwa kufanya vizuri ni Afisa mwanafunzi Taufik Ali Muhsin, huku aliyefanya vyema kwa upande wa taaluma ni Afisa Mwanafunzi Megie mosses Majengo, na kwa upande wa medani ni Afisa kubo mohamed Mwakubo
wengine waliofanikiwa kuzawadiwa zawadi na mheshimiwa Raisi, ni kundi la 72/24- Regular ni pamoja na Afisa mwanafunzi David Mathias Lema, kwenye taaluma ni Kekazuri George Elly, na aliyefanya vizuri katika medani ni Kelvin Samson Isarara
Akiongea mara baada ya kuwatunuku kamisheni Raisi samia alisema kuwa anawapongeza viongozi wa jeshi kwa kuweza kuwafundisha vyema wanajeshi hasa wahitimu kwenye shahada ya sayansi, na wanatakiwa kuendela kusimamia mafunzo kwa wanajeshi ili wawe tayari kwa ulinzi kitaifa na kimataifa.
Dkt Samia alisema mafunzo hayo ambayo wamepata ni muhimu sana kwa maslahi ya nchi, na mafunzo hayo ambayo yanatolewa yataweza kuwasaidia wanajeshi kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa hapa nchini na hivyo kulinda Amani ya nchi.
mwisho




.jpeg)

No comments:
Post a Comment