Hamoud Jumaa awataka vijana kulinda Amani ya nchi yao - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 21 November 2025

Hamoud Jumaa awataka vijana kulinda Amani ya nchi yao




Na Julieth Mkireri,MAIPAC KIBAHA


maipacarusha@gmail.com 


MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa amesema wananchi wanajukumu la kulinda amani yao na kuachana na maneno ya kwenye mitandao ambayo yanavuruga mipango ya maendeleo.


Jumaa pia amesema kama amani ikikosekana na maisha yanaenda tofauti hakuna kitu kitafanyika kwenye jamii.


Mbunge huyo aliyasema hayo Novemba 20 mjinj Mlandizi alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama waliofika kumpokea alipokuwa anatoka bungeni baada ya kuapishwa.


"Sisi wenyewe tuna jukumula kulinda amani yetu tutambue bila amani hatuwezi kuishi tufanye kazi tuachanae na maneno ya kwenye mitandao,"amesema


Kadhalika Mbunge huyo amesema chama kipo imara na wanachama wake hawatakiwi kuohopa tena kuvaa sare zao kwani hali ya amani kwa sasa imeimarika.


Vilevile amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua huku akiahidi kushirikiana na viongozi wa serikali kutekeleza ilani ya chama tawala.


Jumaa amepongeza hotuba ya Rais Samia Sulluhu Hassan aliyoitoa wakati akifungua bunge ambapo pia amepongeza baraza la Mawaziri lililoteuliwa ambalo anaamini litamsaidia Rais katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Naye Diwani wa Kwala Mansur Kisebengo amesema Serikali ya awamu ya sita imepeleka miradi mikubwa katika kata hiyo huku akiomba maboresho kwenye barabara kurahisisha usafiri kwa wakazi wa kata hiyo.


Mwisho

No comments: