MCHAKATO WA KUMPATA MEYA NA NAIBU MEYA WAFUNGULIWA RASMI MANISPAA YA MOROGORO LATIFA GANZEL ACHUKUA FOMU KUGOMBEA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 20 November 2025

MCHAKATO WA KUMPATA MEYA NA NAIBU MEYA WAFUNGULIWA RASMI MANISPAA YA MOROGORO LATIFA GANZEL ACHUKUA FOMU KUGOMBEA


Diwani wa Viti maalumu Latifa Ganzel akiwa emechukua fomu ya kugombea naibu Meya Manispaa ya MOROGORO 



Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


MWANDISHI wa Habari wa gazeti la Uhuru mkoa wa Morogoro Latifa Ganzel amejitokeza na kuchukuwa fomu ya kuwania nafasi ya naibu meya Manispaa ya Morogoro.


Zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi(Ccm) limefunguliwa Leo Novemba 20 na linatarajiwa kukamilika Novemba 21 saa kumi alasiri.


Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Morogoro mjini Khalid Hossein King akiwakabidhi fomu wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hizo kwa niaba katibu wa CCM Wilaya hiyo alisema kuwa zoezi hilo linaendelea na kwamba mwitikio ni mkubwa kwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu hizo.


Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea unaibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Latifa Ganzel ambaye ni diwani wa Viti maalumu alisema kuwa baada ya kulitumikia baraza la Madiwani kwa muda wa miaka 10 ameona sasa ni wakati muafaka wa yeye kugombea nafasi hiyo.


"Mimi kama diwani nimeona ni haki kuwania nafasi hii ya unaibu meya na kipaumbele changu kikubwa ni kwenda kuongeza vyanzo vipya vya mapato ndani ya Manispaa yangu ya Morogoro kwa ushirikiano na meya atakayechaguliwa,"alisema.


Mwisho.





No comments: