Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
WATU wawili wakazi wa kijiji cha Msongozi wilayani Mvomero mkoani Morogoro wamefariki Dunia na wengine nane kunusurika kifo baada ya kula viazi pori vijulikanavyo kama vigonzo.
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa kijiji cha Msongozi kata ya Doma wilayani Mvomero Salehe Saidi alisema tukio hilo lilitokea Novemba 12 Mwaka huu.
Mwenyekiti huyo aliwataja waliofariki Dunia kuwa ni Rajabu Ramadhani na Samweli Kisira na kwamba Novemva 11 mwaka huu Marehemu Rajabu Ramadhani alienda shamba kuchimba vigonzo ambapo inadaiwa alichimba na kitu kingine kinachofanana na viazi hivyo kinachodaiwa kuwa ni sumu.
"Vigonzo hivyo walipandaga, hakugundua kama hicho kingine sumu, aliporudi nyumbani alivipika na kumgawia Samweli na wengine wakala" alisema.
Alisema viazi hivyo aliwapa na majirani zake ambapo baada ya muda walianza kutapika ambapo badae huyo Ramadhani alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro
ilipofika Novemba 12 mwaka huu alifariki dunia
Alisema siku hiyo hiyo Samweli naye alifariki Dunia akiwa nyumbani kwake na kwamba tayari marehemu hao wamezikwa huko Doma.
Mwenyekiti huyo aliwataja walionusurika kuwa ni mtoto wa Marehemu Keila Mohamed, Twahami Amiri, Said Omari, Samia Mwinyimvua, Nasri Doto,Imlagi Said ,Jumanne Salumu na Blaina Joseph.
Kwa upande wake Nafsa Marombwa Daktari hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro aliyekuwa zamu wakati marehemu Ramadhani Rajabu alipofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu, alithibitisha kumpokea ambapo badae hali ilibadilika na kufariki Dunia.
Daktari huyo alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo alikula kitu kinachosadikiwa kuwa na sumu na kuongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea .
Mwisho..

No comments:
Post a Comment