![]() |
| Mkuu Wa mkoa Wa Arusha,CPA Amos Makala |
Na Queen Lema, Arusha
maipacarusha@gmail.com
Mkuu Wa mkoa Wa Arusha,CPA Amos Makala amewataka madiwani Wa halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha kuwa wanawajibika ipasavyo katika kata zao ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato kuanzia ngazi ya kata Hadi jiji.
CPA Makala amesema hayo Leo Jijini Arusha alipokuwa akizungumza na madiwani Wa jiji la Arusha kwenye kikao cha Baraza la madiwani
Pia amewataka kuhakikisha kuwa wanaboresha miundombinu katika vyanzo vya mapato ikiwemo maji,huduma za afya,Ili wananchi walio wengi waweze kutoa mapato.
Alisema kuwa madiwani wanatakiwa wawe na umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu Yao na kuachana na aina yoyote ile ya siasa ambayo inaweza kusababisha ukosefu wa mapato
Alifafanua kuwa nayo halmashauri ya jiji la arusha inatakiwa kuendeleza jitiada mbalimbali za ukusanyaji wa mapato sanjari na kufanya jiji la Arusha kuwa safi Ili kuwavutia wananchi na wawekezaji mbalimbali
Aliwahimiza madiwani kuhakikisha wanasimamia kimamilifu miradi inayotekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao,ili iweze kukamilika kwa wakati
Kwa upande wake diwani Wa kata ya Olasiti Alex Marti amempongeza mkuu Wa mkoa Kwa nasaa zake pamoja na ushauri wake Kwa Baraza la madiwani na kusema kuwa watahakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu Yale walioelekezwa
"Kwa Niaba ya madiwani wenzangu tumeyapokea Yale yote tulioagizwa na mkuu Wa mkoa na tunaaidi kuyasimamia kikamilifu ikiwemo suala zima la ukusanyaji WA mapato,na kuhakikisha jiji linakuwa safi"alimalizia
Mwisho



No comments:
Post a Comment