![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makala akipewa maelezo ya ujenzi wa uwanja wa Afcon |
Na Queen Lema Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu Wa mkoa Wa Arusha CPA Amos Makala amezitaka taasisi za Serikali zote ambazo zinahusika na miundombonu katika uwanja wa mpira wa Afcon kuhakikisha kuwa wanashirikiana Kwa pamoja Ili kuweza kukamilisha mradi huo Kwa wakati
CPA Makala ameyasema hayo Leo wakati akiongea na akikagua maendeleo ya mradi huo Ambao unatarajiwa kukamalika mapema July mwaka 2026.
Alisema kuwa taasisi kama mamlaka ya maji safi ,Tarura, Tanesco,Tanroad wanatakiwa kukaa pamoja ndani ya mradi huo kila siku na endapo kama kuna tatizo waweze kutatua kwa pamoja.
Alifafanua kuwa kwa mara nyingine uwepo wa taasisi hizo nazo zitaweza kuchangia kwa pamoja ukamilishwaji lakini wakati mwimgine taasisi moja inapokosa ushirikiano zaidi ya mwenzake inachangia katizo kubwa
"Kuanzia sasa Taasisi zote za Serikali ambazo zinahusika na mradi huu nawataka muweke kambi hapa mpaka tutakapokabidhiwa maana haiwezekani Auwsa ashindwe kutekeleza uwajibikaji Wake kwa kuwa Tanesco ajatekeleza majukumu yake ipasavyo"aliongeza.
Naye mkandarasi wa mradi huo Denisi Benito alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 70 japo kuwa kwa asilimia 30 Zilizobaki kuna umuhimu wa Serikali kuweza kuruhusu baadhi ya vifaa hasa vinavyotoka nje ya nchi kuingia Kwa haraka
Alisema kuwa wiki chache zilizopita waliweza kuagiza chuma toka nje ya nchi lakini zilikaaa bandarini Kwa siku 21 Jambo ambalo lilifanya utekelezaji kuchelewa
Alibainisha kuwa kwa sasa vifaaa vya ujenzi vilivyobaki vyote vinatakiaa kuingia hapa nchini hivyo basi ni muimu kwa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanalisimamia Hilo ipasavyo
Mwisho


No comments:
Post a Comment