Jaji Chande: Tutafanya uchunguzi huru na kamilifu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 1 December 2025

Jaji Chande: Tutafanya uchunguzi huru na kamilifu




Na Mwandishi Wetu,Maipac

maipacarusha20@gmail.com 

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani baada ya Uchaguzi, imesema itafanya kazi yake kwa weledi na kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote na kwa viwango kwa sababu kazi yao inatazamwa na watu wengi wa ndani na nje yan chi.


Akiongea na waandishi wa habari jinni Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Mohamed Othman Chande, amesema tume hiyo itafanya kazi yake kwa uhuru. Akieleza kuwa hata kabla ya kuanza kazi wao wenyewe wamejiangalia na kutathmini watanzania wanataka nini.


“Tumebaini watu wanataka uchunguzi kamilifu, usifanyike nusunusu, wanataka uwazi kwenye kazi na kama utachukuliwa ushahidi uwe utakaotumika sio ambao hauwezi kutumika,” alieleza Jajic Chande.


Alisema kuwa yako mambo sita ambayo watayafanyia kazi kuwa ni pamoja na kuchuguza na kubaini chanzo halisi cha yaliyotokea, malengo yaliyokusudiwa na waliopanga kutekeleza vitendo hivyo, madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa mali na hasara za kiuchumi zilizojitokeza.


Masuala mengine ni kuangalia mazingira na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na serikali na vyombo vyake, kupendekeza maeneo yahayohitaji kuimarishwa zaidi kuongeza uwajibikaji wa viongozi na raia ili kulinda usalama na utawala bora, utawala wa sheria, haki za binadamu na mfumo madhubuti wa majadiliano ya kisiasa na kijamii hadi kufikia maridhiano na kuhakikisha vurugu hizi hazijirudii tena.


Aliogeza kuwa katika hadidu hizo za rejea wamepewa nafasi ya kuchunguza jambo lolote ambalo tume itaona kuwa ni muhimu na linaendana na majkumu ya tume na kwamba wakiona jambo la iana hiyo hawatahitaji kibali cha mtu kulifanyia kazi.




Amesema tume kama hizo huwa na mwenendo wa kimahakama kwani mtu anapotoa ushahidi anaapa ili baadaye utumike.


Pia, amesema tume hizo huwa huru kuandaa taratibu zake na hazifuati ufundi kama ilivyo katika mahakama na ina mamlaka ya kutoa wito.


“Pamoja na tume kuomba ushirikiano, lakini ina mamlaka ya kushurutisha ushirikiano, lakini sisi hatwendi huko,” amesema Jaji Chande.


Katika ujtekelezaji wa shughuli zao, amesema watatumia njia za mapitio ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali, mahojiano ya ana kwa ana na kwa njia ya mtandaoni, dodoso la mtandaoni, baruapepe, barua za kawaida, kutembelea uwandani, ushauri wa kitaalamu, mijadala ya makundi mbalimbali, simu na jumbe fupi za maandishi.

No comments: