![]() |
| Wakili Jebra Kambole |
Mussa Juma,Maipac
maipacarusha@gmail.com
Arusha. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimefungua Kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki Ikilalamikia kitendo cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzima mtandao kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025 mpaka tarehe 4 Novemba 2025.
Kesi ambayo tayari imesajiliwa katika mahakama hiyo, kwa namba 56 ya mwaka 2025, imefunguliwa juzi na jopo la mawakili wa LHRC wakiongozwa na Jebra Kambole na Peter Majanjara .
![]() |
| Wakili Peter Majanjala |
Katika shauri hilo, LHRC inadai kuwa 29 Oktoba 2025 majira ya saa tano asubuhi, mtandao ulizimwa ghafla kwa ujumla na hii iliathiri Tanzania nzima hadi tarehe 4 Novemba 2025 mtandao uliporudishwa kwenye hali yake ya kawaida.
LHRC imeeleza kuwa, Kuzimwa kwa mtandao kuliathiri watanzania kiuchumi na kijamii kwa kuwakosesha fursa ya kupata taarifa za msingi kwa njia ya kidijitali kama kutumia benki ya mtandaoni, kupata huduma za afya mtandaoni, na kuwanyima mawasiliano. Hii imeathiri uchumi kwa kuleta hasara ya mamilioni ya shilingi.
Pia, LHRC imeeleza kuwa, watanzania walikosa fursa ya taarifa muhumu kuhusu usalama katika kipindi cha kupiga kura, tukio ambalo ni la muhimu kwa taifa.
Serikali ilidai kwamba mtandao ulizimwa kwasababu ya kuzuia vurugu, lakini hii haikidhi matakwa ya kitendo kuwa sawia katika jamii ya kidemokrasia, hakikufata sheria na hakukuwa na haja kufanya hivyo.
LHRC imeiomba mahakama itoe tamko kwamba kuzimwa kwa mtandao kumekiuka vifungu 6(d), 7(2), 8(1)(c) cha Mkataba Unaoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1999.
"Kwamba kuzimwa kwa mtandao kulileta athari kubwa kwa umma, kuzuia Tanzania isirudie tena kuzima mtandao bila kuwa na sheria maalum kuiruhusu kufanya hivyo au bila kuwa na amri ya mahakama"ilisomeka hati ya mashitaka hayo.
Inategemewa kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania atakapopokea ilani ya kufunguliwa kwa maombi kutoka kwa msajili wa mahakama ya haki ya afrika mashariki, atajibu maombi haya ndani ya siku arobaini na tano (45) ili kueleza kisheria kuhusu zuio hilo.
Kesi hii ni ya kwanza kufunguliwa dhidi ya serikali, tangu kuzimwa mtandao ama kupunguzwa kasi jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi mbali mbali hasa wafanyabiashara wa mtandaoni.
Kesi hiyo imefunguliwa wakati tayari LHRC ikishirikiana na baraza la habari Tanzania (MCT), Mtandao wa watetezi wa haki za Binaadamu (THRDC), taasisi ya strategic litigation na mashirika mengine kadhaa yamefungua kesi katika mahakama hiyo, kupinga kanuni za maudhui ya mtandaoni na sheria kadhaa za makosa ya kimtandao kwa maelezo zinakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kulinda uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.
Maamuzi ya kesi hizo yanasubiriwa kutolewa karibuni baada ya majaji wa mahakama hiyo, kusikiliza hoja za wafungua mashitaka na hoja za utetezi za upande wa Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
MWISHO.

No comments:
Post a Comment