![]() |
Na Queen Lema Arusha
maipacarusha@gmail.com
Madiwani 34 kutoka jiji la Arusha wameapishwa rasmi Leo pamoja na kumpitisha Kwa kishindo aliyekuwa meya wa jiji Hilo, Maximilian Iranqhe Kwa Kura 33 na hivyo kuendelea kuongoza baraza Hilo 2025_2030
Akiongea Leo mara baada ya kutangazwa rasmi Meya Maximilian Alisema kuwa bado ana kazi kubwa ya kufanya ndani ya jiji la Arusha
Alisema kuwa Kwa kipindi kilichopita waliweza kufanya kazi nyingi sana za maendeleo lakini pia kufanya kazi kama kiongozi Wa serikali za mitaa ndani na nje ya nchi
Alifafanua kuwa Kwa kipindi kilichopita waliweza kutekeleza miradi mbalimbali lakini bado Ipo ambayo haijalamilika hivyo Kwa kipindi hiki cha Miaka mitano watahakikisha kuwa wameweza kutekeleza miradi hiyo
"Kuna miradi mbalimbali kama ya barabara ambayo inaitaji nguvu ya pamoja katika Baraza hili jipya tutahakikisha kuwa tumeyatekeleza yote"aliongeza
Alihitimisha kwa kuwataka madiwani wote kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi Kwa ujumla
Wakati huo huo mgombea nafasi ya unaibu Meya ,Calling Nathani ,pamoja na Julius ole Sakeyani waliomba kura kwa wmadiwani huku Mshindi akiwa ni Julius ole Sakeyani
Naye Julius Sakeyani ambaye alipata Kura 31 akiongea mara baada ya kushinda kiti hicho alisema kuwa kwa sasa kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa anamsaidia mheshimiwa Meya.
Sakeyani alisema kuwa atahakikisha kuwa anasimamia vyema nafasi yake lakini ili aweze kutekeleza hayo anaitaji ushirikiano mkubwa Baina ya madiwani ,Meya , pamoja na halmashauri Kwa pamoja


No comments:
Post a Comment