Na Julieth Mkireri,MAIPAC KIBAHA
maipacarusha@gmail.com
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani imemkabidhi Tuzo ya utendaji bora wa kazi Meneja wa Wakala wa Barabara wa mkoa huo Baraka Mwambage.
Akikabidhi tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema Meneja Mwambage amekuwa akifanya kazi kwa bidii jambo lililopelekea ofisi yake kutoa tuzo hiyo.
Amesema ofisi yake imekuwa ikitoa barua za kutambua kazi nzuri za viongozi kwenye Wilaya na kwa awamu hii ni mara ya kwanza kutoa tuzo ya kutambua utendaji bora wa kiongozi wa Tasia ya Tanroads.
Kunenge amesema utoaji wa tuzo utakuwa endelevu kwa watumishi watakaokuwa wanafanya kazi kwa bidii kutatua changamoto za wananchi.
Mhandisi Mwambage ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kutambua kazi yake huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kufikia malengo yaliyowekwa katika taasisi yake.
Mwisho.


No comments:
Post a Comment